Sina Mpango wa Kando! Tanasha Donna awaambia mashabiki

Miezi kadhaa zilizopita, Diamond Platinumz na mpenzi wake wa Kenya Tanasha Donna walikuwa hawatenganishwi. Ila mambo sivyo siku hizi kwani wawili hawa wanaonekana kuchapa kazi sana hivyo kukosa wakati wa kuwa pamoja.

Jambo hili limewafanya mashabiki wao ambao huwa wamezoea kuwaona pamoja kuwa na tashwishi kuhusu penzi lao.

Shabiki mmoja alijitokeza na kutaka kujua ikiwa Tanasha bado alikua muaminifu baada kwa msanii huyu wa Tanzania baada ya kuposti video akipitisha wakati na wafanyakazi wenzake.

Aliandika:

''HAWA NDIO AINA YA MARAFIKI NINAO NA HAWA NI SISI KAZINI.''

Tazama video hiyo.

Shabiki mmoja hata hivyo, akiongolea video hiyo alidai kuwa Tanasha anaweza kosa kuwa mwaminifu kwa mchumba wake wa Tanzania.

''NAFIKIRIA DIAMOND ANAFAA KUWA MWANGALIFU SANA,''@HANSMAGAZA ALITOA MAONI.

Diamond na Tanasha waliahirisha harusi yao ambayo ilikusudiwa kufanyika tarehe kumi na nne mwezi wa Februari kwa madai kuwa wawili hawa walitaka kuchukua muda ili waweze kufahamiana vizuri.

Walipatana katika klabu moja jijini Nairobi miaka mbili zilizopita, Diamond akiwa bado kwenye mahusiano ya kimapenzi na Zari(na Hamisa pia) lakini hawakuwa na maongezi wakati huo.

Familia ya Diamond ilimpokea Tanasha vizuri na ilikiri kuwa wamefurahia uamuzi wa Diamond.

Tanasha alichukua muda kutoa woga wa mashabiki kwa kumjibu @hansmagaza.

Alimjibu shabiki huyo kwa upole akisema,

                       ''HANA SABABU YOYOTE YA KUWA NA WASIWASI.''