84875564_485388102134330_6857810328216715778_n

Sina pesa za kupatia watu mimi! Asema Khaligraph Jones kwa mashabiki wanaompigia simu

NA NICKSON TOSI

Khaligraph Jones msanii wa nyimbo za kufoka [Hip hop]nchini ameshtushwa na migerezo ya simu ambazo  anapikiwa na mashabiki wake baada ya jamaa mmoja kutumia akaunti yake ya Twiter na kuandika kuwa atakuwa akiwatunuku baadhi ya wafuasi wake hela.

Akishtushwa na swala hilo Khaligraph aliwaonya wafuasi wake dhidi ya kuamini ujumbe huo uliokuwa umetumwa na mtu ambaye alikuwa ameamua kuwahada wakenya eti atawatunuku watu 30 kila mmoja akipata shilingi alfu 20,000.

Khaligraph alitupilia mbali madai hayo na kusema pia yeye ameathirika pakubwa na mkurupuko wa Corona ambao umeathiri biashara zake na hivyo hana hela za kugawa.

 

Hapa ni ujumbe huo ulikuwa umetumwa na jamaa kwa jina Khaligraph kwenye Twiter.
87653005_205122410604230_3267360358749140775_n
Baada ya kuona jumbe hizo zikienea kwenye Twiter Khaligraph aliandika hivi.
Akaunti ghushi hiyo ,tafadhali msinipigie simu ,niliamushwa na migerezo ya simu tyakriban 200,Corona imetuathiri sisi sote ,hakuna pesa.Aliandika OG

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments