Why i am single!! Nadia Mukami aeleza kwa nini hana mchumba

Msanii Nadia Mukami alifichua kwa nini kwa muda hajakuwa na mchumba maishani mwake. Akizungumza alisema kuwa akiwa katika mahusiano huwa anakwama mahala pamoja na kutofanikisha ndoto zake.

Kwa sababu hiyo Nadia alijipa mwaka mmoja bila kujihusisha na mapenzi wala kukubali uhusiano wowote.

Usemi wake unakuja baada ya shabiki mmoja kumuuliza kama angependa kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake Arrow Bwoy. Kulingana na Nadia amekuwa single kwa muda wa miezi sita na katika kipindi hicho mambo mema na makubwa yametendeka maishani mwake.

Nadia alisema kuwa ana malengo na ndoto za kutimiza na kwa sasa ana ndoto za kutimiza na kutafuta pesa.

“Let me answer this generally as to why I am single!!! I have been single for 6 months and so many great things have happened in a span of 6 months (upgraded). The moment I get in a relationship I swear I always get stuck! Giving myself a one year break! I have some goals I need to attain!! I am an idiot when I am in love! For now I just wanna make money and achieve my dreams!!” Mukami Alisema.

Akijibu swali lingine kulingana atakuwa katika mahusiano lini, alisema kuwa uhusiano atakaokuwa nao utamfanya awe mke wa mtu na wala si uhusiano tu wa kawaida na kuharibu wakati wake.

“The next relationship has to lead to marriage I have been telling my friends I wanna settle down wananishangaa! I don’t like games in relationships I have never dated for fun! Am on a one year break! Immediately I turn 24 all potentials kindly note am ready for marriage kindly note, not a relationship but marriage." Alizungumza.