'Sio kila mtu alimpenda Denno lakini nilijua ametumwa na mungu,' - Faith

IMG_0611 (1)
IMG_0611 (1)
Hivi leo katika kitengo chetu cha ilikuaje, mwanamziki Denno pamoja an mke wake, Faith Naliaka ndio waliokuwa wageni wetu.

Denno amejulikana sana kupitia kwa wimbo wake wa 'Mbona' aliyoimba na mwanamziki Daddy Owen ambaye anakiri kuwa ndiye aliyempa fursa ya kuonesha ubabe wake wa mziki kwa wakenya.

Mke wake Denno jina alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa yeye alimpenda mume wake Dennoe baada ya siku nyingi ya kuwa marafiki na Dennoe na ata alipokuwa tayari kufunga pingu za maisha naye hakusita hata kidogo hata baada ya baadhi ya familia yake.

Faith alisema,

Denno tulipatana church na nilikuwa bestfriend wa cousin yake na alipokuja kumtembelea kanisani ndipo tulipatana. Na kidogo kidogo urafiki wetu ukakua hadi kuoana kwetu.

Alinipata nikiwa katika kipindi kigumu wakati alikuwa amepata ajali na nikapata jeraha kuu na nilikuwa na wasiwasi. Hapo baada ya kupatana na Denno na akanichunga ndipo nilijua kuwa ametumwa na mungu.

Faith pia alikiri kuwa halikuwa jambo rahisi kwa familia yake kumkubali Denno ambaye ni kipofu kama mume wake lakini halikubatilisha lolote.

Nilikuwa naulizwa maswali upande wa familia yangu wakiuliza mbona nilimpenda Denno lakini mamangu alikuwa amekubali chaguo langu na akatubariki kabla kuaga kwake.

Faith anasema shangaziwe alikuwa na shauku yake kumuoa mpenziwe lakini alikuwa ameamua moyoni mwake kuwa atamuoa.

Deno kwa upande wake alifunguka kuhusu maisha ya utotoni na ana bahati kuwa alikuwa anapata upendo kutoka kwa familia yake.

"Nilizaliwa bila uwezo wa kuona na nilipata support sana ya familia. Nilienda shule ya chekechea nikiwa na umri wa miaka sita katika shule ya walemavu Thika. "

Denno anasema licha ya umaarufu wake na kipawa kikuu kuna wakati yeye huwa na shida ya kuzindua muziki na pia jinsi ya kuuneza huwa changamoto.

Hata hivyo anawashukuru wakenya kwani aliporudi baada ya kwenda kimya kwa mda mrefu, wamempokea vyema huku akimshukuru msanii mwenza, Bahati.

Akimshukuru Bahati ambaye pamoja waliimba, 'Story yangu' Denno alifichua kuwa Bahati na mkewe Diana Marua walimzawadi na gari.

"Bahati alinitafuta na tukasign mkataba wa kufanya kazi pamoja, na nataka kumshukuru yeye na mkewe Diana kwani jana alitu surprise na gari."