'Sipendi udaku mimi!' Harmonize atupilia mbali kuwepo kwa uhusiano na video vixen

NA NICKSON TOSI

Msanii wa bongo Harmonize amepusilia mbali madai ambayo yamekuwepo yakimhusisha na Nicole, msichana ambaye alimshirikisha kwa wimbo wake mpya Bedroom, kuwa wamekuwa wakichumbiana.

Akiulizwa katika mahojiano siku ya Jumatano na mtandao mmoja wa Tanzania, Kondeboy kama anavyofahamika na wafuasi  wake alikana madai hayo akisema msichana huyo ni rafiki wake wa karibu na hata wamezaliwa mtaa mmoja wa Mtwara .

Amekuwa rafiki wangu kwa muda hata kabla ya kutoa video hiyo na yeye, waelekezi wangu walinishauri nifanye video hiyo na yeye na kwa sababu nilikuwa natolea video hiyo Afrika Kusini, nilimuuliza iwapo angependa nimshirikishe katika wimbo wangu na kukubali na kutaka nitume tiketi mbili za  Ndege. Moja yake na nyingine ya mchumba wake. Alisema Harmonize

Bifu yaibuka baina ya Harmonize na Diamond kuhusu ni yupi mkali kati yao

Gumzo la Harmonize kuchumbiana na Nicole limekuwepo kwa muda na hata kumfanya msanii huyo kukosana na mpenziwe wa asili ya Kibelgiji.

Kaput! Harmonize  na mkewe  Sarah wablokiana Instagram, Kunani?

Wimbo huo unaoibua hisia mseto miongoni mwa mashabiki ndio huu, tazama.

Kwa sasa, Harmonize amefungua lebo yake ya muziki na kuwasaini wasanii wengine chipukizi kama Ibraah