‘SIR’ Charles Njonjo: Leo anatimu umri wa miaka 100 .

njonjo
njonjo

Umemskia tu au kumsoma katika  vitabu vya histoa na magazeti .Charles Njonjo ni  mojawapo ya watu muhimu sana katika historia ya taifa . Njonjo andiye aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa kwanza nchini na leo anatimu umri wa miaka 100 .Njonjo alikuwa na maamlaka makubwa sana wakati wa utawala wa rais mwanzilishi Mzee Jomo Kenyatta . Baadaye siasa za urithi wa zmee zilipochacha ,Njonjo alimsaidia pakubwa Rais wa Pili Daniel Moi kuwa makamu wa rais na baadaye kuchukua usukani wa  nchi kama rais mwaka wa 1978 mzee Kenyatta alipoaga dunia .

Alivutiwa sana na itikadi na mienendoya kizungu na hata akajipata na  taadhima ya kuitwa ‘The Duke of Kabeteshire’. Njonjo anafahamika sana kwa suti zake zenye mistari na ua katika kifuko cha koti lake . Wakati wa kilele cha maamlaka yake ,Alichosema Njonjo kilichukuliwa kama sharia na kwa bahati znuri alikuwa mshirika wa karibu sana wa Mzee Kenyatta na hata mara si moja amebebwa amoja na rais katika msafara wake rasmi.

Masaibu yake yalimfika mwaka wa 1983  wakati rais mstaafu Moi alipomwona kama tishio na madai ya  yeye  kuwa na njama ya kuipindua serikali ya Moi yakatumiwa kumkata miguu . Katika maisha yake ya kibinafsi hakuwa na mbio za kufunga ndoa na akiwa na umri wa miaka 52,aliweza kumwoa  mpenzi wake ,mwanamke  Muingereza katika kanisa la All Saint Cathedral.  Njonjo alikuwa na kila atakacho  ambapo ufichuzi umetolewa kwamba alikuwa ugali/sima kwa mara ya kwanza alipojiunga na shule yay a Alliance .