Siri ni mihogo na viazi! Museveni afichua kilichomsaidia kupunguza kilo 30

museveni
museveni

Mlo kamili wa mihogo, viazi ulaya na mboga vimemwezesha rais wa Uganda, Yoweri Museveni kupunguza kilo 30, aliiambia BBC.

"Nina afya njema siku zote lakini daktari alionya kuwa nina uzito wa juu hivyo nikaamua kupunguza," bwana Museveni alisema.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 anasema kwamba alikuwa hajazingatia uzito wake ambao uliongezeka hadi kilo 106.

Alikanusha katika mitandao ya kijamii kuwa "anaonekana amechoka" anasema kuwa ni kwa sababu ya kupunguza uzani wake tu ndio maana anaonekana tofauti.

Mwezi uliopita katika blogu yake binafsi, rais Museveni alisema "niliruhusu nikanenepa kwa sababu madaktari walikuwa hawajafafanua vizuri madhara ya kuwa na uzani wa juu".

Aliongeza kuwa uzani wake wa sasa ni kilo 76 ambao ni sawa na urefu wa futi 5(sentimita 170).

Ingawa bwana Museveni hakusema imemchukua muda upi kupunguza uzani kwa jumla ya kilo 30.

"Mini hula viazi kiasi kwa sababu sili kabisa vyakula vya ulaya au Asia. Nala vyakula vyetu tu kama mihogo, ndizi, mtama na mboga zetu za kienyeji,"bwana Museveni alimwambia mtangazaji wa BBC Newsday Alan Kasujja.

" Kwa kawaida huwa ninakula kidogo asubuhi, mchana sili chakula, huwa nnakunywa maji na kahawa bila sukari kwa sababu sukari ni mbaya sana kwa afya," alisema.

"Majira ya saa moja jioni huw aninakula viazi ulaya kwa sababu vina wanga kidogo na ninakula mbogamboga nyingi pia ili kulidanganya tumbo langu kuwa nimeweka kitu kumbe hamna kitu," aliongeza.

Bwana Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986 na ana mpango wa kuwania tena muhula wa sita ifikapo mwaka 2021.

Mwanamziki aliyeamua kuwa mwanasiasa Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 37, anapanga kuwania dhidi yake.

Wiki mbili zilizopita bwana Museveni alitembea kwa kilomita 195 (maili 121) katika mapori ya magharibi mwa Uganda ambako aliwahi kufanya safari za namna hiyo mnamo mwaka 1986 baada ya serikali ya Milton Obote kupinduliwa.

-BBC