'Sitalala na mwanamume mwaka huu.' Asema aliyekuwa mpenzi wa Alikiba

Ali-Kiba-and-Diva
Ali-Kiba-and-Diva
Siku chache zilizopita, mwanahabari wa redio nchini Tanzania Diva The Bause na ambaye alikuwa kipenzi cha msanii wa bongo Alikiba alikiri kuwa walikuwa na uhusiano na msanii huyo japo alikuwa kaoa.

Wawili hao walisemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi wakati Alikiba alikuwa bado amemuoa mkewe Amina Khalef.

Uvumi huo ulienea sana na wawili hao wakakana madai hayo na kisha baadaye Diva alifichua kwamba walikuwa na uhusiano.

Diva alisema kuwa alimtema msanii Alikiba Februari mwaka huu jambo ambalo liliwashangaza wengi na hata kuacha wengi wakisema yeye ndiye sababu ya kutenganisha Alikiba na mkewe.

"ME AND ALI WE CAME ALONG WAY SINCE HIS RETURN IN THE MUSIC WORLD AND YES BOTH AS FRIENDS AND LOW KEY LOVERS FOR A LONG TIME

BY THE WAY I END UP EVERYTHING ON 16/2/2020 AND I TOLD ALI AND I HAVE EVIDENCE AS WELL" Diva Alizungumza.

Ni jambo ambalo lilimfanya Diva kubadili akaunti zake za kijamii, na kisha kusema kuwa hatokuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamume yeyote mwaka huu.

Yote tisa, kumi alisema kwamba hatapekenjeng pia.

"SITAFANTA MAPENZI WALA KUWA NA MWANAMUME MWAKA HUU WOTE WA 2020! IMA STAY SAFE." Alisema.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO