Sitakata tamaa, Mungu pekee ndiye hupeana watoto - Agundabweni

evelyn.wanjiru.agunda
evelyn.wanjiru.agunda
Agundabweni Akweyu, ambaye ni bwanake msanii maarufu wa nyimbo za injili, Evelyn Wanjiry ameidhinisha kuwa mume bora duniani baada ya kutangaza kuwa katu hatokata tamaa kwa ndoa yake.

Hii ni baada ya kufanya mahojiano ya moja kwa moja na tovuti ya Radiojambo.co.ke kuhusu usanii, ndoa yake na pia swala la uzazi.

Miezi kadhaa iliyopita, Evelyn Wanjiru alihojiwa na Massawe Japanni katika kitengo cha Ilikuaje na alifichua kuwa licha ya wawili hao kutopata watoto katika kipindi cha miaka saba, bwanake humpa moyo kila siku.

"Kitu kimoja ambacho hakinipatii hofu ni kujua kuwa mume wangu hunipa nguvu na matumaini kwani najua kulingana na mila za wa Afrika ni kuwa wana ndoa wapya hutarajia kupata watoto baada ya mda mchache." Alisema Evelyn Wanjiru.

Aliongeza akisema,

Najua ni miaka misaba tangia tuoane lakini bado namngoja mwenyezi mungu na naamini atatubariki na mtoto.

Katika mahojiano yetu na bwana Agundabweni Akweyu, tulimuuliza jinsi anavyo chukulia swala la kutopata watoto na kama ashawahi fikiria kukata tamaa na ndoa yake.

Bwana Agundabweni alisema,

La hasha sijawahi fikiria kukata tamaa na ndoa yangu kamwe kwa sababu watoto hutoka kwa mwenyezi mungu na kwa wakati wake atatubariki  na watoto.

Evelyn Wanjiru amezindua kanda mpya iitwayo 'Celebrate' ina nyimbo nane zikiwemo;

1. Celebrate

2. Bless the Lord

3.Holy

4.Jehovah Elohim

5.Its amazing

6.sitaogopa

7.Nanyenyekea

8.I surrender

Hii ikiwa kanda yake ya nne tangia alipoanza taaluma hii, Evelyn alisema kuwa ana furaha mungu amempa uwezo wa kuzindua kanda ya nguvu na ya kufaa. Alisema kuwa kanda hiyo imehamasishwa na mungu mwenyewe.

"Imenichukua miaka miwili kuzindua kanda nyingine mpya na hili ni kwa sababu nyimbo zangu zote huhamasishwa na mungu na pia matokeo ya kila siku." Alisema Evelyn.

Kulingana na mwimbaji huyo wa 'Mungu Mkuu' siri kuu ya nyimbo zake kuwa na maana na kupendwa na wengi ni maombi. Isitoshe anasema kuwa amejifunza kutokimbia studio kuzindua wimbo.

"Nina studio yangu mwenyewe kwa hivyo mimi huchukua mda wangu kuufanyia kazi mziki wangu ili uwe maridadi." Aliongeza.