‘Sitaki ufala, comments za kijinga,’Bien azungumzia ni kwa nini hajawahi kuposti picha za harusi

Msanii wa bendi ya Sauti sol Bien alieleza kwa nini hakuweza kuposti picha za harusi yake na Chikki kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu hakutaka hisia au maoni yasiyostahili.

Wawili hao walifunga harusi yao ya kibinafsi na kuhudhuriwa na baadhi ya marafiki zake na wala si wote.

Akiwa kwenye mahojiano na radio jambo alikuwa na haya ya kusema;

         "HARUSI YANGU HAIKUA HARUSI YA KAWAIDA, NILIENDA KWA AG NA NIKA-INVITE MARAFIKI WANGU WA KARIBU. HIO VIBE ILIKUA HAPO HIYO SIKU ILIKUWA THE HAPPIEST DAY OF MY LIFE. SIJAPATA KUFEEL HIVYO SIKU NYINGINE MAHALI POPOTE PENGINE NA NIKIPIGA PICHA NIEKE MTANDAONI MTU ANAYEANGALIA HIYO PICHA HAELEWI MBONA WATU WAMEVAA VILE WAMEVAA
HAELEWI MBONA BIEN HAJAVAA SUTI. NA SITAKI KUPATIA WATU WAJINGA NAFASI YA KUPEANA MAONI YAO KUHUSU HARUSI YANGU. NITAJIWEKEA, NDIO MSINIHARIBIE HIYO SIKU NA COMMENTS ZA KIJINGA. SITAKI UFALA, VITU ZANGU NI VITU ZANGU."Alizungumza Bien.

Bien alisema kuwa ana hasira za karibu na hakutaka kuwajibisha wakosoaji wake;

"MIMI NI MTU NACATCH FEELINGS HARAKA SANA, NITAJIPATA NATUKANA WATU MARA MTU AMETUKANA MIGUU YA BIBI YANGU MARA AMETUKANA ILE SUTI NILIKUA NIMEVAA."

Bien alisema kuwa hakuna mtu yeyote atakayeona picha hizo;

"WASAHAU, HAKUNA PICHA WATAONA."