'Sitaogopa' Ni wimbo wa kuwapa wakenya nguvu - Evelyn Wanjiru

Msanii wa nyimbo za injili, Evelyn Wanjiru amezindua kibao kipya kwa jina 'Sitaogopa' kibao ambacho kimejia wakti ambao Kenya na dunia nzima imetetemeshwa na virusi vya Corona.

Kulingana na Bi Wanjiru, aliamua kuzindua kibao hiki ili kuwapa wakenya sababu ya kutotishika na kumtegemea mola.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Wanjiru aliwahakikishia mashabiki wake kuwa sote tutashinda majaribio haya.

Isitoshe, aliwakumbusha pia kuwa makini na kujichunga na kuhakikisha wametilia maanani usafi na kusalia nyumbani, ili kuzuia usambazaji wa Coronavirus.

Aliandika,

#Sitaogopa (Live) New music I just released today to encourage you that God is on our side and we will triumph through this season for His glory. Stay safe and remember to observe every safety measures gven by health officials. God bless you all.

Kila siku, ameifanya nia yake kuwapa wakenya kwa jumla moyo na kuwapa nguvu na kuwakumbusha kumtegemea mwenyezi mungu.

When God is on my side

I don't have to be stressed

I don't have to be troubled

What I just do

I put a dance

A song of praise

And I just swerg

Knowing that God is protecting ne

He is covering me

He is always by my side

Tazama kanda ya wimbo wake mpya, 'sitaogopa'