'Sitapiga mikwaju ya penalti tena,' Mshambulizi Sadio Mane asema

sadio.mane
sadio.mane

Mshambulizi wa Senegal, Sadio Mane ametangaza kuwa ataondokea majukumu yake kama mchezaji ambaye hupiga mikwaju ya penalti kwa timu yake ya taifa kwa mda kiasi, baada ya kupoteza mikwaju ya penalti mara mbili mfululizo katika kipute kinacho endelea cha AFCON.

Mane ambaye sasa amefunga mabao matatu katika kipute hicho, alitizama mkwaju wake wa penalti ukiokolewa hapo juzi wakti timu yake ilicharaza Uganda 1-0 katika raundi ya 16 bora, baada ya kupoteza penalti nyingine katika ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Kenya ambapo pia alifunga kwa njia hiyo hiyo ya penalti.

"Naondokea majukumu hayo ila kwa mda mchache tu," Aliaambia wanahabari wa Senegal baada ya mechi hiyo. Nimepoteza mikwaju ya penalti katika mechi hizo mbili na lazima nikubali kuwa sio jambo la kufana."

"Sitaki kuadhibu timu yangu haswa kwa sasa, nitakuwa tu nasimama kando wakti wa penalti ili kuwaachia wachezaji wenzangu fursa ya kuzichapa."

"Nikirudi kwa timu yangu, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii ili ni boreshe mikwaju ya penalti," Aliongeza mshambulizi huyo wa Liverpool.

Hapo awali, mkufunzi mkuu wa Senegal, Aliou Cisse alisema hana shida yeyote iwapo Mane angeendelea kupiga mikwaju ya penalti.

"Yeye hujiamini na ndio maana alipiga ile penalti, alisema. "Lakini haya ni majadiliano ambayo nitakuwa nayo naye."

Mane ambaye amefunga mabao 19 baada ya kucheza mechi 63, anacheza katika kipute cha AFCON kwa mara ya tatu.

-Reuters