Siwezi kufanya kazi na Jubilee - Mudavadi asema

Kiongozi wa chama cha ANC  Musalia Mudavadi amesema hawezi kufanya kazi ama kutengeneza muungano wa kisiasa nchini na chama cha Jubilee .

Hatua hiyo huenda ikawa ni pigo kwa rais Kenyatta ambaye amekuwa akiwazia kufanya marekebisho katika bunge la kitaifa kama njia ya kuwafunga domo wabunge wanaoegemea upande wa naibu rais William Ruto.

Chama cha ANC kina wabunge 17 katika bunge la kitaifa huku kwenye seneti ikiwa na wabunge 3.

“That is their right to act as per their plans. But I want to say there is no enmity, but in matters politics, we as ANC are re-organising and strategising as per the political developments that are taking place in Kenya,” amesema Mudavadi.

Ameongeza kuwa iwapo vyama vilivyoko katika muungano wa NASA havitakuwa vimekubaliana kulingana na uchaguzi wa mwaka 2022, chama chake kitafanya uamuzi kivyake.

“In the NASA agreement, if there is a member party that wants to form another post-election coalition with another, then that party must quit NASA. What is happening in JP are their own internal reorganisation which we are not a party to,” alisema Mudavadi.

Huku Raila akionekana kuingia katika makubaliano ya kufanya kazi na chama cha Jubilee, Mudavadi huenda anawazia kuwa mkuu wa upinzani nchini.

Wachanganuzi wa kisiasa nchini wamesema anapania kuchukua mkondo huo wa kisiasa ifikiapo mwaka 2022 kama njia ya kujiuza kisiasa akisema hataki kivovyote vilie kushirikiana na chama cha Uhuru na Ruto.

Kama njia ya kujipanga vyema kisiasa, Mudavadi amekuwa akishtumu kila mradi wa kiongozi wa taifa na hivi maajuzi amemtaka rais Kenyatta kuweka mipango ya kuhakikisha vijana wanapata kazi baada ya kumalizika kwa virusi vya corona.

"The basic principle is that one cannot belong to more than one coalition at the same time and the law is very clear," amesema Mudavadi.

Kwa upande wake kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ametangaza kuwa chama hicho kitaingia katika mkataba na vyama vingine akisema kiko tayari kujiunga na muungano wa Jubilee-Kanu.

Mbunge wa Lugari Ayub Savula alisema wabunge waliochaguliwa kupitia chama hicho watakutana ili kuangazia mstakabali wa chama.

"Members of ANC will have a final say whether we will quit NASA and join other coalitions or we remain a strong opposition party,"amesema Savula.

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna alisema chama hicho hakichaangazia kivyovyote vile hakijapania kuvunja makubaliano ya NASA .

"The issue of NASA membership was not part of our agenda. We discussed the things that were captured  in our communication,"alisema Sifuna.