Siwezi Fichua Mgombea Urais Wa CORD Hata Unipeleke Kamiti! - Muthama

rsz_muthama
rsz_muthama
Mheshimwa Johnson Muthama alikuwa mgeni wetu asubuhi ya leo, Alhamisi, 6, Oktoba 2016 na baadhi ya aliyozungumzia, moja ilikuwa suala la muungano wa CORD ambao wengi wadai kuwa kuna msukosuko, huku viongozi wa ODM, Wiper na Ford Kenya; Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula mtawalia wakinukuliwa katika mikutano ya hadhara wakijipigia upato kupeperusha bendera ya CORD.

Huku akiwa mwanachama wa Wiper, Muthama ambaye ni seneta wa Machakos alikiri kuwa licha ya chenye wengi wamekuwa wakishuhudia au wanayoamini, muungano wa CORD uko imara na kuwa ni hali ya kufurahia demokrasia.

"Tuna umoja, tuko pamoja na tunapatana lakini demokrasia inatembea kwa wafuasi wa CORD wakiongea jinsi watakavyo." Alisema Muthama.

"Hauwezi laumu anayetaka Joho kuwa naibu wa Raila ifikapo katika kinyang'anyiro cha urais mwaka ujao. Aliangalia akaona huyo ndiye anayefaa. Mimi nataka kuwaambia ya kwamba tumepatana na demokrasia inaendelea." Aliongeza.

Aliendelea akisema kuwa wale wanaokiri kuwa CORD haina mgombea wa urais au gari letu halina dereva, licha ya injini ya gari lile kuguruma wawe na uvumilivu.

"Nataka kuwaambia wananchi kuwa tunashindana na serikali ambayo ina pingu, pesa na vyombo vya uongozi. Ikiwa miezi hii kumi na moja iliyobaki tutaweza kumtoa kiongozi au kinara wetu, Jubilee watamtoboa tumbo hata kabla hajatoka ndani ya nyumba." Alisema.

Kwa hivyo wasubiri tu, dereva tunamjua tushampa funguo tunamtafutia njia vile atapenye.

Kwa hivyo Jubilee wameweka mitego barabarani wanamngojea atokee, atobolewe macho, atobolewe masikio utumbo uteremke chini. Aliongeza akisema kuwa hawezi taja mgombea wao lakini "Siwei mtaja hata ukinipeleka Kamiti, wacha Pangani hata unipe dawa ya kuota."

Skiza kanda ifuatayo huku Mjumbe huyo akizungumzia zaidi kuhusu uhusiano wake na gavana wa Machakos, Alfred Mutua na uvumi kuwa Kalonzo Musyoka aweza kujiunga na chama cha Jubilee hivi karibuni.

&feature=youtu.be