Size 8 afunguka mengi kumhusu babake, alivyotoa msaada kipindi cha ujauzito

singer-Size-8-696x418
singer-Size-8-696x418
Msanii wa nyimbo za injili Size 8 amemzungumzia babake Samuel Kirui Munyali kwa mara ya kwanza.
Size 8 amefunguka kuhusu babake katika mtandao wa Insta akimsifia kwa kutoa usaidizi mkubwa kwake.
Kulingana na muimbaji huyu, Mzee Samuel amekuwa kiungo muhimu cha usaidizi katika masaibu na mahangaiko yaliyomkuta akijifungua.
Katika sherehe ya mtoto wake mchanga, size 8 alilia huku akiwaacha marafiki zake kusononeka zaidi na kumhurumia

Muimbaji huyu alipata mtoto wake wa pili siku chache zilizopita.
"Kwanza nimshukuru Mungu kwa wanaume hawa wawili maishani mwangu. Wamekuwa nami katika maombi na ningetaka Mungu azidi kuwaneemesha..."
"Tena nitoe shukrani zangu kwa wanaume wote wanaosimama kidete na familia zao katika nyakati ngumu za maisha..."
“Mtu yeyote asichukulie sherehe kama hizi kimzaha. Tujifunze kusema shukarani kwa chochote maishani. Kwangu mimi, kufika hapa ni muujiza tu. Nimenusurika kifo mara sio moja. Hata uwe na mabilioni ya hela huwezi kuwa na amani kabisa…”

Haya yanajiri baada ya Size 8 kusimulia masaibu yaliyomkumba hospitalini,

“Nilishtuka sana na nikauliza mume wangu(Dj Mo). Ule ujauzito mwingine uliharibika,je huu ukiharibika kutakwendaje? Kwa hiyo tukaenda hospitali na nikaanza kupata usaidizi…” Alisimulia.