Size 8 ajigamba na kiatu chake ghali Nike Airforce One

Mwimbaji wa nyimbo za injili Size 8 si mwenye mazoea ya kujigamba lakini alilazimika kutuonyesha kitu ambacho alipata hivi karibuni.

Size 8 ni mmoja wapo wa watu wenye kuwa na kiatu orijinali cha rangi ya jeshi Nike Air Force One Sneakers. Kiatu hiki kinaenda kwa dola 200 ambayo ni shilingi elfu ishirini hapa Kenya.

Size 8 alijigamba

               ''hii ni ya kweli, Nike Airforce One, uwe macho kwa zile bandia.''

Hivi majuzi Nike iliweka hadharani picha za muundo mpya wa Air Force One.

Baadhi ya maumbile yanayopatikana kwenye kiatu hiki ni rangi ya kijani iliyotapakazwa vizuri ambayo inaipa njia ngozi inayotanda kwenye upande wote wa juu wa kiatu.

Kiatu hiki ambacho kinasakwa na wengi kina ngozi nyeupe pia kwenye pande zake za kando.

Ama kweli kila mtu na starehe yake.

Tazama video ya msanii huyo akionyesha maumbile ya kiatu hicho.