Soma ujumbe wa Ghost Mulee kwa wanaokejeli kitambi chake

mulee
mulee
Kabla ya mwaka jana kutamatika Ghost Mulee alitangaza mikakati aliyochukua ili mwaka huu wa 2020 aweze kupunguza uzani wake na haswa kitambi chake.

Baada ya kuwa na mwaka wenye mafanikio chungu nzima na sherehe kadha wa kadha ikiwemo kusherehekea miaka 27 ya ndoa, Mulee alisema kuwa lengo lake kuu ni kuboresha afya yake ifikapo mwezi huu wa Februari.

Kupitia mtandao wake wa Insta, Mulee alichapisha kanda akiwa ndani mwa chumba cha kufanyia mazoezi. Katika kanda hiyo Ghost aliwaahidi mashabiki kuwa ifikapo Februari, atavalia mavazi hayo aliyokuwa amevalia ili kuonesha kuwa kwa kweli amejitahidi kupunguza ufuta.

Huku ikiwa tarehe mbili, mwezi wa Februari, 2020, maji nikama yalizidi unga wa Mulee kwani alichapisha picha yake Instagram huku ikiandamwa na ujumbe wa kufurahisha.

Aliandika,

Ooh Ghost punguza tumbo ooh sijui nini??? Be happy with yourself

Swali ni je, kwani Mulee alishindwa kupunguza kitambi na kuamua kujitokeza na kujitetea?

https://www.instagram.com/p/B7--w1dFJOo/