William Ruto

Mbona William Ruto aliamua kupunguza uzito wake.

 


William Ruto huenda ni mmoja wa wanasiasa waliovuma sana humu nchini lakini kuna wakati uzito wake ulitatiza kazi yake kama naibu wa Rais.

Kwa  wakenya ambao huyafuata maisha yake kwa karibu, lazima wamegundua kwamba uzito wake umepungua ukilinganishwa na hapo awali.

Kupitia mahojiano ya hapo awali katika runinga ya Citizen, alisema kwamba aliamua kupunguza uzito wake baada ya kupigwa picha ambayo haikumpendeza.


“I decided to go to the gym after I realised that my weight was getting out of hand…in a specific incident when I had gone to Western Kenya to inspect the problems with sugar (farming), a photograph was taken and it showed me in very bad shape with my tummy protruding,”  Ruto alieleza.

Ruto
Ruto

“A friend called me the next day and told me ‘man you’re doing badly’,” alisimulia.

Baada ya hapo ndipo aliamua kufanya mazoezi kuwa mojawapo ya mipango yake ya kila siku.

Ruto pia amejaribu kumshawishi mkuu wake Rais Uhuru Kenyatta kufanya mazoezi kupitia mbio za mradi wa Beyond Zero ambazo wameshiriki pamoja mara kadhaa.

Mwaka 2019 alikimbia kilomita 21 mfululizo na kumpa changamoto Rais ambaye aliaahidi kushiriki mbio hizo mwaka ujao.

Read here for more

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments