Something cooking! Kiongozi mwingine wa Tangatanga akutana na Mudavadi

RrANzLKk.jfif
RrANzLKk.jfif
Hatua ya kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kuanza kukutana na viongozi wa  mrengo wa Tangatanga nchini huenda inafumbua watu macho kuhusiana na miungano ya kisiasa ambayo huenda ikabuniwa ifikiapo mwaka 2022 wakati wa uchaguzi mkuu.

Mudavadi hii maajuzi alikutana na viongozi wengine akiwemo Moses Wetangula wa Ford Kenya, Gavana wa Jackson Mandago wa Uasini Gishu na mbunge wa Sirisia John Waluke, mikutanoa  ambayo ilitazamiwa  kama ya kubuni miunganao ya kisiasa nchini.

Wakati kiongozi huyo wa ANC anapoendelea kuwambia watu kuwa hakuna miungano yoyote ya kisiasa inayobuniwa nchini, wageni ambao wamekuwa wakizuru katika boma lake inaibua hisia mseto sana.

Mandago na Waluke wote ni mashabiki wakubwa sana wa naibu rais William Ruto ambao wamekuwa wakisema watampigia debe ifikiapo mwaka 2022, wakati wa uchaguzi mkuu.

Kiongozi wa sasa kuzuru katika afisi za kiongozi huyo wa ANC ni mbunge wa Kimilili Dismus Barasa ambaye ni shabiki mkubwa sana wa Ruto.

Wawili hao wamefanya mkutano wa kisiri eneo la Mudavadi Center ambapo maswala ya siasa na miungano yalitawala.

"This morning Kimilili MP Didmus Baraza paid me a visit,We discussed among other things the unfolding political events in the country, matters of elementary democracy and lastly, strategic and visionary plans to revive the ailing economy,"  amesema Mudavadi.