Soma hadithi nyingine:
Cherangany MP Joshua Kutuny amekuwa wa kwanza kutangaza na kusema kuwa njia iliyotumika kwa kweli inahujumu demokrasia. Kulingana na mbunge huyu, wagombeaji wote 16 walipaswa kufanyiwa mchujo wa kina kabla chama kimtangaze nguli huyu wa soka.
Soma hadithi nyingine:
Katika chapisho rasmi mtandao wa Facebook, Kuria alisema atamuunga mkono Musungu kwa sababu yeye ni mzaliwa wa Kibra huku akimfananisha na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo marehemu Ken Okoth. Alisema kwamba kiongozi aliyezaliwa Kibra anafahamu shida na changamoto za wakaazi wa eneo hilo na ana nafasi nzuri kuboresha maisha ya watu wa eneo hilo.
Soma hadithi nyingine:
“Rafiki yangu Ken Okoth alizaliwa Kibra na alikuwa amejitolea sana kuimarisha maisha ya watu wa Kibra. Mtu ambaye nitapigia debe kuendeleza mipango ya Okoth ni mzaliwa mwingine wa eneo hilo, Benson Musungu,” Kuria alisema
Sasa uteuzi wa Mariga umesababisha tumbo joto katika chama tawala na wengi wanahoji kuwa chama hicho kifutilie mbali uteuzi huu.