Sonko akosekana Mahakamani Voi, adaiwa kuwa na matatizo ya kiafya

Sonko lawyers in Voi-compressed
Sonko lawyers in Voi-compressed
Gavana wa Nairobi Mike Sonko amekosa kuhudhuria mahakama ya Voi kutokana na madai kuwa na matatizo ya kiafya.

Sonko alitakuwa kusomewa mashtaka yake leo kutokana na madai ya kuwashambulia maafisa wa polisi Disemba 6.

Gavana huyo ametakiwa kuwasili tena kortini Januari 21, 2020.

Ripoti ya daktari iliyowasilishwa kortini inaonyesha kuwa' Sonko ana shinikizo la juu la damu pamoja na maumivu kifuani.'

Wakili wake George Kithi anasema kuwa mteja wake atawasili kortini kama jinsi alivyoagizwa na jaji.

Sonko anakumbwa na mashtaka 19 ya ufisadi, utumizi mbaya wa mamlaka na ubadhirifu wa shilingi milioni 357 kwenye kaunti ya Nairobi.

Awali, hali ya usalama ulidumishwa katika eneo la mahakama kutokana na umati mkubwa uliowasili kushuhudia kesi hiyo ya Sonko.

Baadhi ya wawakilishi wa kaunti ya Nairobi walihudhuria kusikizwa kwa kesi yake kortini.

Gavana anadaiwa ‘kumpiga teke’ kamanda wa polisi wa kanda ya pwani Rashid Yakubu kwenye paja lake alipokuwa akikamatwa kwenye uwanja ndege wa Ikanga.

Katika kesi hiyo, gavana atafunguliwa’ shtaka la kumshambulia afisa wa polisi akiwa anatekeleza wajibu mnamo Disemba 6.”

Sonko anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwashambulia na kuzuia maafisa wa usalama kutekeleza wajibu wao kazini

Na shtaka la pili ni “kukataa kutiwa mbaroni na Yakubu..na kukaidi amri ya kuabiri helikopta ya polisi.”

Aidha, gavana anatuhumiwa kutumia cheche za matusi kama vile,” shenzi nyie, taka taka, ondoka hapa, akiwa na lengo la kuhujumu amani.”

Kulingana na orodha ya mashtaka yanayomkabili yaliyoandikwa Disemba 9, Sonko anatuhumiwa kuwashambulia polisu saa 12.30 adhuhuri na kuwazuia kutekeleza wajibu wao ipassavyo kulingana na sheria za tume ya huduma za polisi 2011, ibara ya 103.