Sonko aomba msaada kutoka Uhuru, asema mambo magumu Kaunti ya Nairobi

Sonko
Sonko
Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko ameomba msaada kutoka rais Uhuru Kenyatta kukabiliana na magenge ambao wanamzuia kutekeleza shughuli zake kikamilifu.

Mike Sonko amejitetea kwamba ilibidi awatimue kazi baadhi ya maafisa katika idara ambazo haziajibikii kazi zao ipasavyo.

"Ile cartel iko hii Nairobi ni kubwa zaidi, nahitaji msaada wako kudismantle." Sonko alisema.

Sonko ametoa wito kwa rais kumsaidia kukabiliana na magenge wanaomzuia katika utendakazi wake.

“Lakini rais ile cartel tunajaribu kudismantle hii Nairobi itafika mahali mweshimiwa rais uingilie," Sonko amesema.

Sonko alikiri kwamba mkasa wa Precious Talents School  ambao ulisababisha maafa ya wanafunzi wanane ulitokana na uzembe wa maafisa wake wa kaunti.

Aidha Gavana alisema kwamba anapanga kuwatimua maafisa wengine ambao ni wafisadi.

Sonko alisema kwamba juhudi zake za kukusanya mapato ya kaunti yamesambaratishwa na magenge ambayo hupora pesa hizo.

"Vile ulifanya KRA ukapeleka wafisadi nyumbani, naomba msaada wako. Nairobi kama ni revenue chukua huko national government," Sonko alisema.