Sonko na mkewe watimiza miaka 21 ya ndoa

104226477_318956535798903_1094803310026597312_n
104226477_318956535798903_1094803310026597312_n
Japo yupo chini ya shinikizo haswa baada ya kutimuliwa kutoka kwa afisi zake City Hall, Mike Sonko anasalia kuwa na furaha na kuendeleza familia yake kwa furaha.

Sonko na mkewe Primerose wameadhimisha miaka 21 ya ndoa na akitumia fursa yake, mkewe Primerose aliandika katika mtandao wake kumshukuru mumewe kwa kuendelea kuijali familia yao kwa miaka hiyo yote ambayo wamekuwa pamoja kama mume na mke.

Alimtakia mumewe Sonko maadhimisho mema ya ndoa saa chache tu baada ya Sonko kuwashauri wanaume kuwajibikia majukumu yao kama wazazi.

Primerose alitundika picha yao wakiwa pamoja na akiwa amekalia karibu na Sonko, picha ikiashiria penzi lao halisi.

Miongoni mwa watu wanaomfuatilia walimpongeza kwa kuishi kwa ndoa miaka hiyo yote na kumtakia kila heri.

Katika ujumbe huo, Sonko alifunguka na kusema kuwa japo hakuna mwanadamu aliyemkamilifu duniani, mafanikio yake kwenye ndao yao ni kusema neno Sorry anapokuwa amekosea.

Amewahimiza wanaume kuomba msamaha iwapo wamekosea katika uhusiano na wakati wanapotofautana na wake wao.

 "If your wife catches you with a side chick say sorry, If you return home late say sorry. If you are wrong always say sorry," Sonko.