Sonko Na Peter Kenneth Wanafaa Kuunda Serikali Ya Nusu Mkate Jijini Nairobi - Mureithi

francis mureithi
francis mureithi
Huku siku zilizobakia kabla ya siku ya upigaji kura nchini zikididimia, joto la kisiasa limeanza kupanda huku wawaniaji wakijitosa ulingoni katika juhudi za kuonyesha umaahiri wao katika uongozi.

Tukisalia jijini Nairobi, kiti cha ugavana ni mojawapo ya vinyang'anyiro ambavyo vitatifua vumbi zaidi kwani kimevutia wawaniaji wengi wakiwemo, Gavana Evans Kidero, Seneta Mike Sonko pamoja na aliyekuwa mgomneaji wa urasi mwaka wa 2013, Peter Kenneth.

Hivi majuzi bwana Sonko alinukuliwa katika runinga ya Citizen akisema kuwa kamwe hawezi ng'atuka kama muaniaji wa kiti hicho ili amuachie bwana Kenneth akidai kuwa pia yeye alikataa kung'atuka ili amuache rais Uhuru Kenyatta nafasi ya kuwania urais uchaguzi uliopita.

Hayo yakiwa mambo yanayozungumziwa, wengi wamejitokeza kupeana maoni na hata pendekezo zao huku anaye wania kiti cha ubunge Embakasi Mashariki, bwana Francis Mureithi akipendekeza kuwa wawili hao waweza fanya kazi pamoja.

Kulingana na bwana Mureithi ambaye atakuwa akiwania kiti kile kwa mrengo wa Jubilee iwapo atashinda kura ya uteuzi, alidai kuwa wawili hao waweza ungana na kuunda serikali ya nusu mkate jijini Nairobi.

"Heri kusema ukweli hapa, Seneta wa Nairobi na Peter Kenneth ni wanachama wetu wa Jubilee, na hao wawili wana msukumo mkubwa hapa Nairobi kwa sasa wale wengine akina Margaret Wanjiru sioni umaarufu wao saana katika hicho kinyang'anyiro cha Nairobi. Kwa hivyo kile tungependa kuhimiza kama wanachama wa Jubilee tungependa Seneta na Peter Kenneth wafanye kazi pamoja ili tuweze kushinda kiti cha Nairobi."

Alisema Mureithi katika mahojiano ya moja kwa moja na watangazaji Gidi na Ghost Asubuhi.

"Kwa hivyo Seneta na yeye wanatakikana wasikilizane, wakae chini wakubaliane hata kama wangeweza kuunda serikali ya nusu mkate Nairobi kwa sababu sasa ni wetu wote. "

Aliendelea bwana Mureithi, ambaye pia atamenyana na aliyekuwa kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi, Babu Owino katika kiti cha ubunge wa Embakasi mashariki.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be