Sonko wa masonko azuru Kirinyaga na Embu na kuzawadi mashabiki sugu

IMG_20190806_092829[1]__1565098841_55646
IMG_20190806_092829[1]__1565098841_55646
Sonko wa masonko hii leo asubuhi ametua mji wa Kerugoya na kuwapa zawadi mzomzo mashabiki wa kaunti ya Kirinyaga. Kwa siku 2 mfululizo kituo cha Redio Jambo kimepiga kambi kaunti hiyo. Jana, sonko huyo alitua Mji wa Gurubani Mwea na kuwapa mashabiki hela kibao.

Soma hapa:

Swali rahisi kabisa la kutambua The Phrase That Pays ndilo linaloulizwa ili shabiki aweze kung'amua kuwa ni Redio Jambo Ongea Usikike na mara moja anakutunuku elfu moja. Iwapo maneno haya sonko atayaona kwenye bango basi elfu 5 pesa kibao zaidi. Sonko anatarajiwa kuzuru mjini Meru kesho na kutembea viunga vyake ili kugawa hela kwa mashabiki.

Pata uhondo hapa:

Watu kutoka maeneo yanayozunguka mji wa Meru hapo kesho watafurahi zaidi kukutana na sonko kutoka redio inayoongoza nchini kwa matangazo na vipindi bora zaidi ya Jambo.Ikumbukwe kuwa zoezi hili linatarajiwa kuendeshwa hadi mwisho wa mwezi wa Agosti. Kwa sababu ikiingia wiki ya 4 tangu lilipoanza.

Mashabiki kutoka sehemu za Ukambani wanatarajia kutembelewa na kituo hiki juma lijalo. Sonko atakuwa anachana kabisa kaunti za Machakos, Makueni na baadaye Taita taveta.