Uhuru aomba radhi - Rais aomba msamaha wakenya kutokana na ukatili wa polisi

NA NICKSON TOSI

Rais Uhuru Kenyattta siku ya Jumatano aliomba msamaha kwa wote walioathirika na dhulma za polisi kutokana na amri ya watu kutotoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa 11 asubuhi.

Akizungumzia matukio hayo Kiongozi wa taifa alielezea masikitiko yake kuhusiana na visa hivyo ambapo wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi walidhulumiwa na maafisa wa polisi, hatua iliyofanya wengi kukashifu mienendo ya polisi.

Haya yanajiri saa chache tu baada ya mtoto wa miaka 13 Yassin Moyo kudaiwa kuuawa na polisi eneo la Kiamaiko katika mitaa ya mabanda ya Mathare kisa ambacho kilikashifiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini.

Maeneo mengine yaliyoshuhudia visa kama hivyo ni Mombasa katika kivukio cha feri cha Likino ambapo maaafisa wa polisi walinaswa wakiwapiga wanawake kabla ya muda wa makataa uliowekwa na serikali kutimia.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO