Mhariri mkuu wa kimataifa Michael Slackman akijibu video yenye ucheshi kukejeli tangazo la kazi hiyo amejitetea akisema wamejitolea kuchapisha na kuueleza ulimwengu kuhusu matukio ya bara afrika lakini sio kwa ajili ya dhana dhalilishi na udunishaji wa maisha ,mfumo wa uongozi na uendeshaji wa masuala ya waafrika . Wiki jana New York Times ilichapisha tangazo ikisema inamtafuta mwandishi anayefaa kuwa mwepesi wa ‘kurukia ‘ taarifa ili kutangaza kuhusu mizozo , na pia kuvutiwa na taarifa za upekuzi .
Tangazo hilo halikuwapendeza watumizi wa mitandao ya kijamii
“Our Nairobi bureau chief has a tremendous opportunity to dive into news and enterprise across a wide range of countries, from the deserts of Sudan and the pirate seas of the Horn of Africa, down through the forests of Congo and the shores of Tanzania,” Ilisoma sehemu ya tangazo hilo kwa lugha ya kiingereza .
Lakini Slackman ambaye hapo awali amewahi kufanya kazi Cairo, Berlin, Moscow, Albany na Melville amekiri kuhusika na uandishi wa tangazo hilo na amesema anajutia kwa kutochukua muda ufaao kutayarisha maelezo yanayokubali ya akina ya waandishi na kazi waliofaa kuifanya badala ya kutumia maneno yaliotafsiriwa kulidunisha bara la afrika .