Sossion awashauri walimu kutii agizo la kurejea shuleni

Sossion
Sossion
Muungano wa walimu nchini Knut  umewataka walimu kutii agizo la w mwajiri wao TSC la kuripoti  shuleni siku ya jumatatu .

Tume ya kuwajairi walimu TSC jumatatu iliwaagiza walimu wote kuripoti shuleni kufikia jumatau wiki ijayo kwa matayarisho ya kufunguliwa kwa shule  .

Siku ya jumanne  Wilson Sossion  ambaye ni  katibu mkuu wa KNUT amesema walimu  wako tayari kuokoa muda uliopotezwa wakati wanafunzi walipokuwa nyumbani kwa sababu ya janga la corona baada ya shule kufungwa mwezi machi .

" Nawahimiza walimu kujitolea kwa udi na uvumba   na kujituma kuliko walivyowahi kujituma kwa sababu tupo katika kipindi kisicho cha kawaida’ amesema Sossion .

Aliyasema hayo katika makao makuu ya muungano wa KNUT wakati wa  uzinduzi wa kampeini ya uhamasisho kuhusu kukabiliana na dhulma za kijinsia .

Muungano huo umesema uamuzi wa kubadilisha kalenda ya shule umechukuliwa kwa sababu visa vya maambukizi ya ugonjwa wa corona vimepungua .

Miongoni mwa watakaohitajika shuleni ni  ni walimu  .Hawa ni pamoja na wale walio na Zaidi ya umri wa miaka 58 na walio na matatizo ya kiafya

Hapo awali TSC ilikuwa  imesema kwamba walimu hao wenye umri wa Zaidi ya miaka 58 na wenye matatizo ya kiafya wangesalia nyumbani

Sossion amewataka walimu kufuata kikamilifu mikakati iliyowekwa na wizara ya Afya  katika kupambana na virusi  vya corona wakati shule zitakapofunguliwa .

Zaidi ya walimu 380,000 watarejea kazini  huku  tarehe ya wanafunzi kurejea shuleni ikikosa kujulikana hadi kufikia sasa .