Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi ajiuzulu

Elachi
Elachi
Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi amejiuzulu .Elachi   amesema kwamba  amechukua hatua hiyo kuendelea na siasa  za eneo bunge la Dagoretti kaskazini .

“  Wakati waliopita niliondoka kichwa changu ikiwa chjini lakini kwa sasa naondoka kwa fahari’ amesema Elachi

Naibu wake ambaye pia ni mwakilishi wa wadi ya  Ruai John Kamangu sasa ndiye atakayechukua nafasi hiyo .

“ Kwa unyenyekevu nawasilisha  kujiuzulu kwangu kwa rais Uhuru Kenyatta .siku chache zilizopita zimekuwa na visa vya kutishia masha .namteua naibu wangu John Kamangu kuwa kaimu spik’ amesema Elachi .

Elachi  alimshukuru rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa nafasi ya kuwahudumia wakaazi wa Nairobi kwa miaka mitatu iliyopita  na akaongeza kwamba anatamanai sana kuhudumu katika utawala wake katika nafasi nyingine hivi karibuni .