Sportpesa na Betin zashinda kesi dhidi ya KRA

Makampuni ya kucheza kamari ya Sportpesa na Betin yameshinda kesi dhidi ya KRA kuhusu kiwango cha ushuru kinachotozwa kwa kila senti inayoshindwa na wateja.

KRA imekuwa ikidai mabilioni kutoka makampuni haya hususan kutoka ushuru unaotozwa  fedha zinazowekezwa pamoja na zile zinazoshindwa na wateja.

Uamuzi wa korti unaonekana kuunga mkono makampuni ya Sportpesa na Betin huku ikizuia kiwango cha asilimia 20 cha ushuru.

Uamuzi wa korti  ulipinga  ushuru wa asimilia 20 kwa pesa ziliozoshindwa na mteja ikiwemo pesa zilitumiwa na wateja kucheza kamari.

Marekebisho yalifanyiwa kipengee hicho awali ambacho ushuru ulikuwa ukitozwa kwa kiwango pesa zilizozawidiwa washindi pekee bila kujumuishwa na pesa zilizokusanywa kutoka wacheza kamari.

Hata hivyo, kipengee hicho kilijumuisha jumla ya fedha zote zilizoshindwa na mteja pamoja na kiwango cha awali kilichotumiwa katika kucheza kamari.

Sportpesa na Betin pamoja na makampuni mengine ya kucheza kamari yalifungwa kutokana na kanuni mpya iliyowekwa na serikali kuhusu ushuri unaotakina kutozwa.

Kanuni hizo mpya ziliwekwa ili kudhibiti mchezo huu wa uraibu ambao serikali inasema imewateka vijana wengi sana.