Sportpesa yaagiza wafanyakazi kurejesha barua za kufutwa kazi, Je kuna matumaini ?

Kampuni ya Sportpesa imeamuru wafanyakazi wake waliochishwa kazi  mwanzoni mwa mwezi huu kuzirudisha  barua hizo.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Ronald Karauri aliiambia Radio Jambo kwamba waliamua kuwaagiza wafanyikazi wote kurejesha barua hizo ili kupewa zingine zinazoambatana na sheria za leba.

"Tumeagizwa kutoa notisi halali na inayowiana na sheria  wakati tungali twasubiri bodi ya kutoa leseni na kudhitibiti kamari kushughulikia matakwa yetu," Karuru alisema.

Oktoba 2, Sportpesa ililazimika kuachisha kazi zaidi ya wafanyakazi 400 baada ya kutangaza kusitisha shughuli zake hapa Kenya kutokana na kile kampuni hiyo ilataka kama sheria dhalimu za utozwaji kodi.

Hata hivyo Sportpesa haikufurahia hatua ya serikali kuongeza ushuru hadi asimilia 20 kwa pesa anazoshinda mteja.

"Kuongezwa kwa kiwango hiki cha ushuru kutawanyima wateja pesa zao wanaozishinda na ktalemaza juhudi za kuwekeza katika spoti nchini," taarifa kutoka kampuni ilisema.

Hata hivyo, kampuni hiyo ina matumaini ya kurejesha tena huduma zake wakati serikali itakapolegeza masharti yao na kufanya mazingira kuwa bora kwa biashara.

Kufungwa kwa kampuni kulilemaza juhudi za kufadhili vilabu vya soka nchini.

Soma taarifa nyingine:

(Mhariri Davis Ojiambo)