SportPesa yakanusha madai ya kusitisha shughuli zake nchini

KARAURI
KARAURI
Kampuni ya kucheza kamari SportPesa imekanusha madai kwamba inapanga kusitisha shughuli zake kufuatia hatua ya serikali kudinda kuidhinisha leseni yake.

Kampuni hiyo ilisema inaendelea na mazungumzo na serikali na wadau wengine kupata suluhu kwa utata uliyoko na ambao umepelekea kusitishwa kwa oparesheni za makampuni mengine 26 ya kamari.

Habari zaidi:

“Tunaimani tutarejelea shughuli za kawaida hivi karibuni,” Taarifa ya SportPesa ilisema.

Kampuni hiyo ilisema kwamba taarifa zote kuhusu oparesheni zake zitatolewa kupitia njia rasmi.

Oparesheni za SportPesa zimesitishwa tangu Ijumaa wiki iliyopita baada ya serikali kuagiza makampuni ya huduma za mawasiliano kufunga nambari maalum za malipo za kampuni hiyo kwa madai ya kukwepa ushuru.

Habari zaidi:

Sportpesa na mashirika mengine 26 ya kucheza kamari na ubashiri yalitakiwa kutuma upya maombi ya kutata leseni za kuhudumu kwa lengo la kunasa wakwepaji ushuru. Ili kuonyesha kujitolea kwa serikali kulainisha sekta ya kucheza kamari nchini, waziri wa maswala ya ndani Fred Matiang’i aliwafurusha wakurugenzi 17 raia wa kigeni wa mashirika ya kamari.

Wakurugenzi hao wengi wao kutoka Mashariki mwa bara ulaya, wanadaiwa kujihusisha na biashara tofauti na zile zilizoko katika vibali vyao vya kufanyia kazi.  Ripoti zimeonya kuwa mamia ya watu watapoteza kazi ikiwa serikali itashikilia msimamo wake dhidi ya mashirika ya kucheza kamari.

Wengi wa wanaokabiliwa na tishio la kupoteza ajira ni maafisa wa kiufundi katika mashirika hayo, maafisa wa kushughilika wateja na wale katika idara za masoko katika vituo vya mashirika hayo.