Staa wa bongo Harmonize atangaza kuzamia siasa 2020,

Screenshot_from_2019_12_31_12_20_18__1577784055_99260
Screenshot_from_2019_12_31_12_20_18__1577784055_99260
Sasa ni bayana kuwa staa wa Bongo Fleva Harmonize atazamia siasa za ubunge mwaka ujao.

Konde Boy ambaye kwa sasa ameshika nafasi nzuri kwenye game ya muziki Afrika mashariki na ya kati amefanya tangazo hilo kupitia mtandao wake maridhawa wa Insta.

Staa huyu aliwatangazia mashabiki waliokuwa wamejaza uwanja eneo la Tandahimbab alipozaliwa Harmonize.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alikuwa wa kwanza kutoa tamko la kumtaka staa huyu agombee ubunge wa Tandahimba,

Nchi jirani ya Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi mpya mwaka ujao.

Nyota ya Harmonize inazidi kung'aa zaidi baada ya kuitema lebo ya WCB.

Harmonize almaarufu kama Konde Boy amekuwa mkubwa kwa kupiga nyimbo hatari na kushirikisha mastaa wakubwa kutoka nchi jirani kama Uganda na Nigeria kati ya nyinginezo.

Matamasha anayoyafanya ni makubwa sawa na bosi wake Diamond Platnumz.

Ana walinzi sawa na idadi ya Diamond.

Kumewahi kutokea vyombo vya habari nchini Tanzania zinazowalinganisha wawili hawa.

Ila je,unafikiri muziki wa Harmonize utashuka akizamia siasa?