'Stay in your lane please!Ringtone amuita Akothee'Wazimu'

akothee2
akothee2
Mwanamuziki Akothee ameweza kuenea sana katika mitandao ya kijamii kwa wanachi kusema kuwa hakuwa amevalia nguo mzuri wakati alipokuwa akitumbuiza mashabiki wake.

Kilicho wafanya wananchi kukasirika ni wakati ambapo aliweza kufungua miguu yake wazi mbele ya mashabiki wake ilhali wazazi wake walikuwa katika maeneo hayo ya kuwatumbuiza mashabiki.

Maoni ambayo waliweza kuandika katika mitandao ya kijamii walisema kuwa Akothee si mfano mwema wa kuigwa anaye tarajiwa na kizazi cha vijana.

Akothee hakuweza kunyamaza bali aliweza kujibu na kusema,

"Miguu iko kwa ajili ya kupanuliwa na nilipanua nikiwatumbuiza mashabiki shida iko wapi? Nina lipwa kwa ajili ya kufanya hivyo,

"Na kweli nikua naenda benki kuweka pesa ambazo nililipwa mwishoni mwa wiki juu ya kipindi hicho," Akothee alijibu.

Mwanamuziki Ringtone alikuwa amefikwa koo na wazimu wake na kuomba kupitia njia ya mtandao, akiomba kwa niaba ya mashabiki wa Roysambu.

Akimwambia Akothee kuwa aweze kukwamilia kwa kucheza, kuimba na kuacha wazimu kwa watu ambao ni wazimu.

"Akothee mashabiki wamenituma kwako wanalalamika, wanasema kuwa huwezi kuwa muimbaji mwenye mafanikio, mchezaji ambaye pia amefanikiwa na mwanamke wazimu ambaye amefanikiwa,

"Na huwezi fanikiwa kwa kila kitu. Achia wazimu kazi yao. Akothee kuwa katika mstari wako wa kuimba na kucheza kwa maana uwezi fanikiwa kuwa wazimu, achia wazimu wafanye kazi yao,"Aliandika Ringtone.

Kama watu wengi wanavyo mjua mwanamziki Akothee uwa anajibu ukosoaji na maneno makali mno mbayo unafikiria mara mbili katika maisha yako ama ni wewe au mtu mwingine.

Katika maoni ya wananchi wameweza kumuonya mwanamuziki Ringtone kuwa siku yake haitaisha vizuri endapo Akothee ataweza kumjibu katika usemi wake.

Waliweza pia kumuambia kuwa endapo mwanamuziki huyo ata jibu ataweza kujuta kwa nini aliweza kusema maneno hayo kumuhusu.