Step by step:Mwanahabari Maribe alikuwa na Sonko wakati Monica alipouawa-Shahidi

Jackie Maribe kiwa kortini
Jackie Maribe kiwa kortini
Kwa Mukhtasari

  • Sonko Alikuwa ameratibu mkutano na Jeff Koinange
  • Rafikiye Maribe aiambia mahakama kwamba walikuwa kituoni  hadi Sonko alipomaliza mahojiano yaje na wakaondoka saa tano unusu usiku  pamoja na Maribe  hadi eneo la burudani la  Club 40/40, Westlands. Walisalia huko hadi saa Kumi alfajiri .

Mtangazjai wa zamani wa habari  Jacque Maribe  alikuwa na gavana wa Nairobi Mike Sonko  siku ambayo Monica Kimani aliuawa ,mahakama ilielezwa  siku ya jumatano . Mmoja wa mashahidi katika kesi ya mauaji ya Monica  ,rafiki ya Maribe  Chelagat Ruto  ameiambia korti kwamba Maribe alikuwa pamoja na Sonko usiku wa mauaji hayo .Ruto alisema kwamba  septemba  tarehe 19 mwaka wa 2018  alienda eneo la  Road House Grill  na rafiki yake mmoja mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni  na walikutana na Joseph Irungu al maarufu Jowie  akiwa na rafiki yake .Walipata chakula cha mchana . Maribe na mpenziwe wa zamani Jowie  wameshtakiwa kwa mauaji ya Monica Kimani ,shtaka wanalokanusha .Ruto  anasema Jowie alikuwa na  kaptula  ya rangi ya brown yenye mifuko ya pembeni   na kofia ya rangi ya  maroon  na Tshirt ya rangi nyeupe . Waliitisha nyama choma  na viazi  na kula pamoja wakipiga gumzo . Chelegat amesema Jowie alikuwa akibugia kileo cha Vodka na rafiki yake ilhali naye alikunywa maji . Amesema alikuwa huko kumtayarisha Sonko  kwa mahojiano yaliopangwa katika kipindi cha JKL  usiku huo. Mwendo wa saa mbili unusu usiku , Jowie  na rafiki yake wa kiume waliondoka sehemu hiyo  na akamtumia rafiki yake Juliet pesa kupitia huduma  ya Mpesa  kulipia  bili .Ruto   alisema alikutana na Maribe mwaka wa 2017 wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu  ambapo alikuwa katika kundi la  kampeini za seneta  Johnson Sakaja .

Ameiambia mahakama kwamba baadaye walikuuza urafiki  na Maribe  alimtambulisha kwa Jowie .Mahakama  iliambiwa kwamba mwendo wa saa tatu usiku aliondoka Road House Grill na kuliegesha gari lake jeupe   la Range rover  katika eneo la Q lounge  linalokaribiana na  afisi za Royal Media services . Waliingia katika jumba hilo la  habari  na kumpata Sonko ,wakamtayarisha kwa mahojiano  na walipokuwa katika  ukumbi wa kungojea watu ,walikutana na Maribe aliyekuwa akifanya kazi .Ruto ameiambia magakama kwamba  walikuwa kituoni hapo hadi Sonko alipomaliza mahojiano yake na wakaondoka saa tano unusu usiku wakiwa na Maribe kwenda 40/40 mtaani Westlands.Ruto  amesema walikuwa  Club 40/40  pamoja na Sonko  hadi mwendo wa saa saba usiku wakati Jowie alipojiunga nao .Walisalia huko hadi mwendo wa saa kumi alfajiri .

Jowie  alielkea katika meza waliokuwa na kuwasalimu kabla ya kurejea katika meza ndogo ya watu wawili na kuagiza  Tusker Lite. Ameiambia mahakama kwamba aliondoka kilabuni humo pamoja na Juliet katika gari lake  ilhali Maribe aliondokana katika gari lake pamoja na Jowie . Alisema siku chache baadaye alipata habari za kuuawa kwa mwanamke mmoja katika nyumba yake mtaani Kilimani . Amesema alishangazwa  kwamba Jowie na Maribe ambao hawakuwa na tofauti zozote naye walihusishwa na mauaji hayo . Msimamizi na mfanyikazi wa bustani za nyumba za Lamuria Apartments pia  walitoa ushahidi wao . Msimamizi huyo  Reagan Buluku  na mfanyikazi wa shambani  Stephen Wanjohi  wote walisimulia jinsi walivyoupata mwili wa Monica .

Mahakama ilifahamishwa kwamba walikuwa wakitoka kwa chakula cha mchana septemba tarehe 20 na kukutana na  kakake Monica George pamoja na mchumbake .George  anaripotiwa kumtaka Buluku amsaidie aingie katika nyumba ya dadake kwa sababu hakuwa  akichukua simu   na baadaye simu hiyo ikazimwa .Buluku  alisema kwamba walipofika katika nyumba ya Monica ,runinga ilikuwa imewashwa na maji yalikuwa yakisikika yakitiririka kutoka mferejini .Buluku  kasha alimwambia Wanjohi kuleta ngazi  ili waweze kuifikia ghorofa ya tatu   ili waweze kuifikia nyumba ya Monica kupitia Jikoni . Wanjohi aliitumia ngazi hiyo na kuingia chumbani mwa Monica kupitia dirishani .Anasema hakuweza kumwona Monica  popote  na  pia alikuwa akiutafuta ufunguo  ili aweze kuufungua mlango ili mradi awawezesha wengine kuingia katika nyumba ya Monica . Anasema alielekea katika chumba cha kulala   lakini hakumwona yeyote  licha ya kutazama sehemu nyingine za   nyumba nzima .Baadaye aliamua kwenda   kuangalia  bafuni . Aliuona mwili wa Monica  ukiwa katika tabu ya kuogea .maji ya mfereji yalikuwa bado yanamwagika katika tabu hiyo .

Kulingana na msimamizi na mfanyikazi wa shambani ,mikono yake yote na miguu ilikuwa  imefungwa na koo lake kukatwa ,na kuongeza kwamba kuliwa na damu katika shingo lake .Wanjohi  alipiga kamsa na  kuwaambia waliokuwa nje wauvunje mlango kwa sababu  mambo hayakuwa mazuri mume ndani .Buluku alipata kifaa cha kutumia na wakavunja mlango  kasha wakaingia katika nyumba ya Monica .