STILL FRIENDS? RAIS Uhuru na naibu wake Ruto wakutana kwa mara ya kwanza baada ya mwezi mmoja

  Rais  Uhuru Kenyatta  na naibu wake William Ruto wameonekana pamoja   hadjharani kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya mwezi mmoja siku ya jumapili .wawili hao walihudhuria hafla ya  kasisi Abraham  Mulwa kuchukua uongozi wa kanisa la AIC milimani .

Pombe ya Bure:Jamaa wakimbilia kupora  pombe baada ya lori la kubeba vileo kuanguka

Kabla  ya hafla hiyo ,rais na naibu wake walionekana  hadharanai pamoja  disemba tarehe 19  wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri . Kumekuwa na ripoti kwamba uhusiano kati yao umevurugika sana na huenda ushirikiano wao kisiasa umefika tamati . Naibu wa  rais hata hivyo amekanusha hilo akisema yungali ana uhusiano mzuri  na rais Kenyatta .

Akiwahutubia waumini katika kanisa hilo  rais aliahidi kuendelea kushirikiana na kanisa katika kuihudumia jamii . Hatua yao ya kuhudhuria hafla moja iliwapata wakenya kwa ghafla  kufuatia  uvumi kwamba huenda urafiki wao wa karibu umeathiriwa kwa ajili ya mgawanyiko ulioshuhudiwa mwanzoni kuhusu siasa za mwaka wa 2022 na ripoti ya BBI . Mambo yalizidishwa wakati  rais alipolifanyia mabadiliko baraza la mawaziri akiwa Mombasa bila kuandaman na naibu wake kama ilivokuwa ada wakati wa muhula wao wa kwanza .