Stop it! Yvonne Okwara apata usaidizi wa 'General'Miguna

Mtangazaji wa  Runinga ya Citizen  Yvonne Okwara  alijipata pabaya baada ya jeshi la mtandao KOT kumshambulia vikali kwa ajili ya kauli yake kuhusu hatua ya baadhi ya watumizi wa mitandao kusambaza picha za utupu za Brenda Cherotich ambaye alipona virusi vya Corona .

Yvonne alikuwa akitoa maoni yake lakini wengi katika KOT hawakuwa tayari kuheshimu maoani yake na wakageuza patashika zima kuwa shambulizi la ndani na masuala ya kibinafsi huku wengine hata wakipiga mashimo katika ndoa yake na taaluma yake  katika uanahabari .

Baada ya msururu wa mashambulizi hayo kuna ‘Jenerali’ mmoja ambaye aliibuka kwa ujasiri kuja kumtetea  Okwara . Miguna  Miguna kupitia twitter aliwashauri wanatwitter kuhehsimu demokrasia na uhuru wa kila mtu kutoa maoni yake bila kumvamia kuhusu masuala ya kibinafsi lakini ushauri huo uliingia katika sikio lililozibwa .

Miguna aliwashauri wanaomkosoa Okwara kufanya hivyo kupitia njia ya maoni yao na ushahidi bali sio kubinafsisha suala hilo kwa kuanza  kumpaka tope kuhusu maisha yake ya ndoa na wengine hata kuanza kukosoa maumbile yake .