Sudan: Abdalla Hamdok ateuliwa waziri mkuu

Abdalla Hamdok
Abdalla Hamdok
BBC

Sudan imemteua Waziri Mkuu mpya ikiwa nchi hiyo ikiwa kwenye utawala wa mpito wa miaka mitatu chini ya uongozi wa jeshi.

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok anasema kuwa kipaumbele chake ni upatikanaji wa amani na kutatua changamoto ya kiuchumi .  Uteuzi wake umekuja wakati ambapo Luteni Abdel Fattah Abdelrahman Burhan alichaguliwa kuwa kiongozi mpya wa baraza huru.

Serikali mpya itaongoza taifa hilo mpaka kipindi cha uchaguzi. Kumekuwa na vurugu kwa miezi kadhaa ambayo imesababisha vifo vya waandamani wengi.  Upande wa upinzani una matumaini kuwa uteuzi mpya utaweza kusaidia kumaliza utawala wa kijeshi. Migogoro nchini Sudan ilianza kwa waandamanaji mwishoni mwa mwaka jana wakati ambapo Omar al- Bashir alipoondolewa madarakani baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 30.

Bwana Hamdok ameapishwa kama waziri mkuu wa mpito alipowasili kutoka Ethiopia, eneo alilokuwa akifanyia kazi kama mtaalamu wa uchumi wa umoja wa mataifa(UN) tangu mwaka 2011 kabla ya kuacha kazi hiyo mwaka jana.

"Vipaumbele vya kwanza vya serikali ni kusitisha vita, kuimarisha usalama, kuuza uchumi na kujenga uhusiano mzuri na sera za mataifa ya kigeni," aliwaambia waandishi wa habari.

Mwaka jana, Hamdok alichaguliwa na Bashir kushika nafasi ya waziri wa fedha lakini alikataa, shirika la habari la AFP.

Kuapishwa kwa Hamdok na uwepo wa baraza huru inaonyesha utofauti kwa mara ya kwanza tangu Sudan ikiwa haipo chini ya utawala wa kijeshi tangu Bashir aingie madarakani mwaka 1989 . Baraza huru inachukua nafasi ya utawala wa mpito wa majeshi wakati ambapo utawala wa kiislamu ulipoondolewa baada ya maandamano makubwa.

Gen Burhan atawaongoza viongozi sita wa kiraia na wengine wanne wa kijeshi kama mpango wa wa muda mrefu wa miezi 39 kuelekea kwenye demokrasia.