Sumu iliyowakosa Shanice na Michael, mamake Joyce Syombua asimulia

Mamake Joyce Syombua amesimulia tukio nzima la jinsi mshukiwa Peter Mugure alifanya jaribio la kuwapa sumu watoto Shanice, 10 na Michael, 5.

Akizungumza na runinga ya Citizen, Elizabeth amefunga A-Z jinsi tukio hilo lilifanyika.

“Kuna kipindi walikuwa wanatoka shule. Wakapatana na mama aliyesema alikuwa mwalimu wao huko LakeWood. Akawanunulia maandazi na soda. Akawafungulia. Na huyu mdogo Mike alikuwa very keen,”  Alisema.

“Alisema aliona mama akiweka kwa soda kitu inakaa strungi. Hawakunywa. Kufika kwa nyumba mama yao alikuwa amewaachia funguo. Kuenda kuchange nguo mama mwingine akakunywa hiyo soda. Akafaint. Hata akaishiwa na nguvu hakuwa anaongea. Mtu wa duka aliconfirm aliuzia hao watoto hiyo soda.” Alizidi kusimulia.

Peter Mugure ni mshukiwa mkubwa anayepelelezwa ili kubaini muuaji wa watoto hawa pamoja na mamake.

Watoto wanadaiwa kuwa wake Peter Mugure baada ya uthibitisho vinasaba au DNA.

Mahakama iliamuru kuwa anatakiwa kuwapa usaidizi na kufadhili malezi ya watoto hawa.

Vita hivi vimepelekea kuwapoteza mama na watoto wake.

Miili ya Joyce, Shanice na Michael ilipatikana na makachero Jumamosi katika makaburi yaliyopo umbali na mji wa Nanyuki.