Taarifa ya Habari Alhamisi Tarehe 3 Oktoba ,Toleo la Saa Moja

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imesema imeanzisha uchunguzi wa madai kwamba  baadhi ya maafisa wa serikali wanashikilia uraia wan chi mbili .ingawaje EACC imesema katiba inaruhusu wakenya kuwa raia wan chi nyingine , sheria kuhusu kuhusu  maadili  ya uongozi inawazuia baadhi ya watumishi wa umma dhidi ya kuwa na uraia wa mataifa mengine .

Mahakama ya leba imemzuia kwa muda  jaji mkuu dhidi ya kuwaapisha makamishna wapya wa tume ya kitaifa ya mashamba . uteuzi wa makamishna hao uliidhinishwa jana na rais Uhuru Kenyatta kupitia arifa ya gazeti rasmi la serikali kwa  muhula mmoja wa miaka sita .

Kuviadhibu  vyama vya ushirika vya matatu kwa ujumla kwa ajili ya makosa  ya  mwanachama mmoja  ni ukatili na adhabu kali sana isiofaa . mwenyekiti wa jopo la rufaa la bodi ya kutoa leseni  Andrew Kimani amesema  NTSA badala yake inafaa kuwaadhibu wanachama a wanaofanya makosa .

Sarah Wairimu  amekana  mashtaka ya kumwua mumewe Tob Cohen .wakili wake Philip Murgor  ameruhusiwa kuendelea kumwakilisha  katika kesi hiyo  .wakati huo huo Peter Karanja  amefikishwa  kortini  huku mawakili wake wakitaka afanyiwe ukaguzi wa kiakili kabla ya kujibu mashtaka ya mauaji ya Cohen .

Muungano wa walimu Knut umeunga mkono hatua ya serikali kuzifunga shule zenye majengo yasio salama  na zile ambazo hazina leseni za kuhudumu . katibu mkuu WILSON  Sossion  amesema shule  475 za Bridge international zinafaa kufungwa kwnai hazijasajiliwa kwa njia ifaayo.

Hakikisha kwamba upo katika eneo salama wakati wa upepo mkali .bernand shanzu kutoka idara ya utabiri wa wa hali ya anga  amesema wanaoishi katika mitaa ya mabanda wanafaa kuepuka nyumba zisizo thabiti ili wasijeruhiwe .

Chanjo ya HPV itakayzinduliwa nchini itatolewa kwa wasichana  walio na umri wa miaka kumi na itatolewa kwa dozi mbili  ,moja baada ya miezi sita .Collins Tabu kutoka wizara ya afya  amesema uamuzi wa kuwachanja wasichana hao wakiwa na umri wa miaka kumi ni  kwa sababu hawana virusi vya HPV vinavyoambukizwa kupitia ngono .

Takriban watu wawili wamethibitishwa kuaga dunia baada ya jengo la ghorofa  mbili linalojengwa huko Butali ,kakamega kuporomoka .idadi isiojulikana ya  wafanyikazi katika jengo hilo wamenaswa na vifusi .shirika la msalaba mwekundi na wananchi wanashirikiana kuwaokoa  wafanyikazi hao.