Vijana wametahadharishwa dhidi ya kukubali kugawanya na wanasiasa .rais Uhuru Kenyatta amesema vijana wanafaa kuzingatia ustawi wao na wa nchi bila kujali makabila yao kwa lengo la kuhakikisha kwamba mustakabali wao ni mzuri .
Waziri wa elimu George magoha amesema marekebisho katika vyuo vikuu lazima yatekelezwe kwani haisadii kuwa na vyuo vikuu vingi vinavyotoa ubora wa chini wa elimu . magoha amesema heri kuwa na vyuo vikuu vichache vinavytoa elimu bora
Gavana wa Taita Taveta granton samboja atajua hatma yake katika kipindi cha siku 10 zijazo wakati kamati ya senate ya wanachama 11 iliyoundwa kuchunguza kufurushwa kwake afisini itakapotoa ripoti yake . kamati hiyo itaangazia lalama zilizoibuliwa dhidi ya samboja ikiwemo kukosa kutoa mwongozo kuhusu utayarishaji wa bajeti.
Kiongozi wa Thirdway Alliance Ekuru Aukot amelaumu ufisadi , ubarakala wa kisiasa na vitisho kama sababu zinazowafanya waakilishi wa kaunti kuukata mswada wake wa punguza mizigo . Aukot ameashiria kwamba huenda akaelekea mahakamani ili kupinga sababu zinazotolewa na mabunge ya kaunti kuukata mswada huo .