Taarifa ya Habari Toleo la saa Kumi

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
 

 TAKRIBAN  asilimia 20 ya wapiga kura  wameshapiga kura katika uchaguzi mdogo wa wadi ya  ganda huko kilifi .afisa msimamizi wa uchaguzi  Juma Musa amesema  wengi wamezuiawa kufika vituoni kupiga kura kwa ajili ya mvua iliyoanza kunyesha leo asubuhi .

Maseneta wamezuiwa kujadili  au kuendelea na mchakato wa   kushughulikia hoja ya waakilishi wa bunge la taita taveta kumwondoa afisini gavana granton samboja hadi kesi ambayo gavana huyo amewasilisha kortini isikizwe na kuamuliwa . samboja amesema maseneta walipuuza agizo la awali la mahakama na kuunda jopo la kuchunguza madai yaliyotolewa dhidi yake .

Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha okook kaunti ndogo ya teso kusini  HUKO  busia baada ya mwanafunzi mmoja wa kike wa kidato cha kwanza katika  shule ya upili ya mseto ya  st  .Mark  machakus kuuawa  baada ya kupigwa na radi .jenipher amoit anasema kuwa mwanawe lydia emwatok alipigwa na radi nyumbani kwao saa moja jioni alipokuwa  akianika  sare zake za shule.

Mbunge wa malindi Aisha Jumwa na mlinzi wake  wameagizwa  kufika mbele ya DCI  jumanne wiki ijayo  ili kuwasaidia  katika uchunguzi  kuhusiana  na rabsha zilizotokea katika wadi ya ganda na kupelekeea kuuawa kwa mtu mmoja . wameachiliwa kwa dhamana  kwa ajili ya ukosefu wa ushahidi .

Baadhi ya barabara  mjini Mombasa hazipitiki kwa ajili ya mvua kubwa  inayoshuhudiwa katika eneo hilo .idara ya utabiri wa hali ya anga  imesema kiasi cha mvua  kitazidi  huko pwani  hadi jumapili .

Wanafunzi  wawili waliopotea  kutoka shule ya  wavulana ya utumishi  huko gilgil  wamepatikana  wakiishi hapa Nairobi  na binamu zao  baada ya kutafutwa kwa wiki mbili . wawili hao ambao ni watahiniwa KCSE walitoweka kutoka shuleni humo katika hali ya kutatanisha .