Taarifa ya Habari Toleo la saa saba 23/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
Mahakama ya leba imefutilia mbali uteuzi wa Mary Wambui kama mwenyekiti wa maamlaka ya ajira  . hii ni baada ya  seneta wa Nairobi Johnson sakaja  kuwasilisha kesi kortini kupinga uteuzi huo .

Watu wawili wameaga dunia  baada ya lori lao kutumbukia katika mto  Mtwamwogodi  katika barabara ya   Voi-Mwatate .kamanda wa kaunti ndogo ya   Mwatate Monicah Kimani s amesema lori hilo lilikuwa likielekea mwatate kutoka Voi  wakati dereva alipopoteza mwelekeo na kugonga vizuizi pembeni mwa mto huo .

Watu wanne  wamekamatwa  baada ya kutibuliwa kwa njama yao ya kuiba  pesa katika benki moja huko Ruiru . wanne hao walikuwa wakipanga kuiba pesa katika mashine ya ATM ya benki ya Barclays  ,Ruiru  , mkuu wa DCI George   Kinoti amesema . washukiwa hao ni Hillary Ng'eno( kutoka KK security), Jared Nyang'au(G4S), Douglas Momanyi ( mhudumu wa boda boda )  na Jacob Barasa.

Iwapo umeathiriwa na mvua inayoshuhudiwa katika sehemu nyingi za taifa ,basi usiwe na hofu kwani usaidizi upo njiani .waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa  amesema serikali itasafirisha kwa ndege bidhaa za matumizi na vyakula kwa takriban watu 1000 walioathiriwa na mafuriko katika kaunti nane . Victor Simani na maelezo

Mtumie daktari mmoja  endapo mpendwa wako atapatikana  na ugonjwa wa kansa  .mtaalam wa ugonjwa huo Philip Odiyo  amesema matibabu ya kansa ni utaratibu wa muda mrefu na uhusiano wa karibu kati ya mgonjwa na daktari  ni jambo muhimu katika kuhakikisha kwamba  mwathiriwa anapata nafuu kwa haraka .

Serikali za kaunti zimeshauriwa kuwalipia watu walio na umri wa miaka 70 na zaidi ada za  bima ya matibabu ili wapate usaidizi wa matibabu . naibu mwenyekiti wa SUPKEM Mohamed washalla  amesema watu wengi wa umri wa juu katika kaunti wanateseka kupata matibabu kwa ajili ya hali yao ya  umaskini .