Taarifa ya Habari Toleo la saa Saba 28/10/2019

RADIO JAMBO MIC
RADIO JAMBO MIC
 Ndege ya kampuni ya silverstone imelazimika kutua kwa dharura  katika uwanja wa  ndege wa eldoret  baada ya gurudumu lake moja kuanguka ikiwa hewani  .Ndege hiyo iliyikuwa na abiria wanne na wafanyikazi watano ilifaulu kutua kwa njia shwari katika uwanja huo ambao ulitayarishwa kwa  hali yoyote pindi tukio hilo liliporipotiwa kutoka uwanja mdogo wa ndege wa  Lodwar ambako ndio hiyo ilikuwa ikitoka .

MAHAKAMA kuu imekataa kutoa agizo la kuziruhusu serikali za kaunti kununua dawa kutoka kwa   wauzaji wengine wa dawa isipokuwa shirika la dawa nchini KEMSA .JAJI WELDON Korir  amelikabidhi suala hilo kwa jaji mkuu atajayetaja jopo la  majaji wa kuisikiliza na kutoa uamuzi  kuhusu kesi hiyo . kesi hiyo inapinga  uamuzi wa kulitaka shirika la KEMSA kuwa  pekee linaloziuzia kaunti dawa .

Halmashauri ya utunzi wa mazingira nchini NEMA  imeagizwa kutekeleza notisi ya kuyafunga maeneo ya burudani ya Kiza, B club na Space Lounge mtaani Kilimani  baada ya wakaazi kulalamikia  kuchezwa kwa muziki wa sauti ya juu  katika sehemu hizo za burudani .

Matayarisho ya mtihani wa KCPE   yanakamilishwa hivi leo kote nchini kabla ya mtihani huo kuanza hapo kesho ,.huko North rift  usalama   umeimarishwa katika vituo vyote vya kuanyia mtihani  hasa  katika sehemu ambazo huathiriwa na visa vya wizi wa mifugo

IWAPO Mgonjwa wa kansa  anaamua kukueleza masaibu anayopitia akiugua ni vyema kusikiliza badala ya kulinganisha hali yake na yako au ya mtu mwengine . mtaalam wa kansa Philip Odiyo  amesema kulinganisha hali ya mgonjwa mmoja hadi mwingine  sio jambo la busara kwani kila mmoja ana  vitu tofauti alivyopitia .

 Rais Donald Trump  wa marekani ametangaza kwamba kiongozi aliyekuwa akijificha wa kundi la Islamic State , Abu Bakr al Baghdadi alijiuwa mwenyewe wakati wa uvamizi wa kikosi maalum cha Marekani nchini Syria. Katika tangazo la runinga , bwana Trump alitangaza kwamba gaidi huyo nambari moja duniani amefariki wakati wa uvamizi hatari wa usiku kaskazini magharibi mwa Syria na vikosi maalum vya Marekani.