Baadhi ya barabara mjini Mombasa hazipitiki kwa ajili ya mvua kubwa inayoshuhudiwa katika eneo hilo .idara ya utabiri wa hali ya anga imesema kiasi cha mvua kitazidi huko pwani hadi jumapili .
Wanafunzi wawili waliopotea kutoka shule ya wavulana ya utumishi huko gilgil wamepatikana wakiishi hapa Nairobi na binamu zao baada ya kutafutwa kwa wiki mbili . wawili hao ambao ni watahiniwa KCSE walitoweka kutoka shuleni humo katika hali ya kutatanisha .
Mswada wa punguza mizigo umefeli na sasa wakenya wanafaa kuangazia jitihada za jopo la BBI . baadhi ya viongozi wanaounga mkono BBI wamesema jitihada hiyo ndio njia bora kwa taifa kwani maoni ya wakenya wote katika kaunti 47 yalichukuliwa .
Mbunge wa malindi aisha jumwa Aisha jumw ana mlinzi wake wameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi laki tano pesa taslimu au bondi ya shilingi milioni moja kila mmoja .mahakama imekataa kuwazuilia kwa siku 21 kama ulivyotaka upande wa mashtajka kwa ajili ya kukosekana kwa ushahidi kuhusu mashtaka ya kuchochea ghasia .
Waziri wa afya Sicily kariuki amefika mbele ya kamati ya bunge kuhusu afya ili kutoa maelezo kuhusu ununuzi wa vifaa vya matibabu uliosababisha kupotea kwa mabilioni ya pesa za umma . kariuki amewaeleza wabunge hatua kwa hatua kuhusu utaratibu uliofutwa katika ununuzi huo kuanzia mwaka wa 2015 .
Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja amewasilisha kesi kuzuia kuteuliwa kwa mary wambui kama mwenyekiti wa maamlaka ya ajira .amesema wambui hana tajriba ya a angalau miaka saba katika uajiri na usimamizi wa wafanyikazi ili kushikilia wadhfa kama huo kama inavyohitajika sheria .