TABIA MBAYA!Betty Kyallo alalama kuhusu tabia ya wafanyikazi wa nyumbani kuiba hata wakilipwa shilingi 18,000 .

Betty-Kyallo-smiling
Betty-Kyallo-smiling
  Mtangazaji wa runinga Betty Kyallo ameonyesha ghadhabu yake na mtindo wa mayaya wa nyumbani kufanya wizi majumbani walikoajiriwa licha yaw engine kulipwa vizuri .Mtangazjai huyo wa habari wa K24  Alionekana kuhamakishwa na tabia hiyo na kuyapeleka  manung’uniko yake katika  ukurasa wake wa instagram .

Kyallo alikuwa akilalama kwamba badahi  ya ‘maids’ bado wana tabia mbaya  ya kuwaibia waajiri wao licha ya kuwa wanalipwa hata shilingi elfu 18 kwa mwezi!.

 Haijabainika iwapo Betty amekuwa mwathiriwa wa tabia hiyo mbaya ya wafanyikazi wa nyumbani lakini uchungu wake unaweza  kueleweka na waliowahi kuathiriwa na ukatili unaofanywa na wafanyikazi kama hao. Kyallo amewarai wazazi kupitia ujumbe wake wawe waangalifu  kuhusiana na wafanyikazi wa nyumbani na  kutowaamini kwa asilimia 100 na kila jambo nyumbani .