TABITHA.1 (1)

Tabitha Karanja na mumewe waachiliwa kwa dhamana

Wakurugenzi wa kampuni ya Keroche Tabitha Karanja na mumuwe Joseph Karanja wameachiliwa kwa dhamana baada ya kufikishwa katika mahakama ya Milimani kujibu mashtaka ya ufisadi siku ya Ijumaa.

TABITHA.1 (1)

 

Tabitha Karanja aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 15 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au shilling milioni 10 pesa taslim. Mumewe Joseph Karanja aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au shilingi milioni mbili pesa taslim.

Ufisadi! Wakurugenzi wa Keroche wafikishwa kizimbani

Hakumu mkuu Francis Andayi hata hivyo amewapa siku saba kuwasilisha dhamana zao mahakamani. Mahakama hata hivyo imewaagiza wasalimishe paspoti zao. Wawili hao ambao walikamatwa Alhamisi baada ya kulala katika majengo ya kampuni hiyo walikanusha mashtaka yote kumi dhidi.

 

 

Tabitha alikesha katika korokoro ya polisi baada ya kuandikisha taarifa katika idara ya DCI, mumuwe Joseph Karanja hata hivyo aliachiliwa kwa dhamana ya polisi kutokana na hali yake ya kiafya.
Wakurugenzi wa Keroche wanadaiwa kukwepa kulipa ushuru wa takriban shilingi bilioni 14 pesa za Kenya.

 

 

Katika taarifa siku ya Jumatano, Karanja alisema kampuni yake haijashiriki ukwepaji wowote wa ushuru na kuongeza kwamba haikua haki kwa kampuni ya Keroche “kuhujumiwa na kudhalilishwa”

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments