'Tafadhali nisaidie,' Ledama Ole Kina amwambia Raila

EXZ-RMFXYAAuq9d
EXZ-RMFXYAAuq9d
Seneta wa Narok Ledama ole Kina amelazimika kumlilia kinara wa ODM Raila Odinga ili kusaidia kulinda nafasi yake ya mwenyekiti wa kamati ya uhasibu kwenye seneti.

Ledama alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo bila kuungwa mkono na chama chake.

ODM baadaye ilipinga matokeo ya uchaguzi huo na hata kumwandikia Spika na kumuondoa Ledama kwenye kamati hiyo.

Ledama alisema kuwa  Raila ana uwezo wa kutatua mzozo huo kwa hivyo anahitaji usaidizi wake.

“Nataka kumuuliza kiongozi wangu wa chama kuwa ushindi wangu unaibiwa, tafadhali niunge mkono." Alizungumza Ledama.

Aidha licha ya ODM kutangaza nia ya kumuondoa kwenye kamati hiyo, kiongozi huyo aliendelea kuwa mkaidi.

"Mambo yatakuwa mabaya kwa sababu hatuwezi kuendelea kutengwa na kuwa tu wa kushabikia hali."

Chama cha ODM kilikuwa kina muunga mkono Sam Ongerikuchukua wadhifa  wa mwenyekiti wa PAC.

Duru ziliarifu wanachama wa ODM kwenye kamati hiyo walikuwa wamekutana na kinara wao Raila Odinga na kuagizwa kumchagua seneta Sam Ongeri kama mwenyekiti.

Iliarifiwa Ledama aliungana na Millicent Omanga, Mithika Linturi, Kimani Wamatangi (Kiambu), na Hargura Godana (Marsabit) na ndipo akamshinda Ongeri.