Orodha ya makocha waliofutwa kazi baada ya AFCON

Herve Renard anajiuzulu kama kocha mkuu wa Morocco baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika kashindani ya kombe la mataifa ya Afrika.

Morocco ni mojawapo wa timu zilizopigiwa upatu kabla ya kuanza kwa mahsindano hayo Misri 2019 lakini ilishindwa kupitia mikwaju ya penalti na Benin katika timu 16 za mwisho.

AFCON: Algeria ndio mabingwa wa bara Afrika

Renard, raia wa Ufaransa amewahi kushinda mataji mawili ya Afcon na Zambia (2012) na Ivory Coast mnamo 2015, alikiongoza kikosi cha Morocco tangu Februari 2016.

“Umwadia wasaa wa mimi kuufunga ukurasa huu mrefu na mzuri katika maisha yangu,” amesema Renard mwenye miaka 50.

Katika taarifa kwenye mtandao wa kijamii, Renard amesema “Ni uamuzi usioweza kuepukika ulichukuliwa hata kabl aya kuanza mashindano ya Afcon 2019.

“Nilichukua uamuzi huu- bila shaka – baada ya kutafakari kwa makini. kwahivyo siwezi kuugeuza.”

Renard aliitoa Morocco kutoka nafasi ya 81 katika orodha ya Fifa duniani hadi katika nafasi ya 47.

Hatahivyo Renard siyo kocha wa kwanza kuondoka au kuondolewa kutokana na matokeo duni katika mashindano hayo yaliokamilika mwaka huu.

Wanyama kupambana na Salah katika michuano ya kufuzu AFCON 2021

Amunike

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) mapemamwezi Julai limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike.

Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo.

“Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019,” ilisema taarifa ya TFF.

Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018.

Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39.

Mastaa watano wakiafrika walioshindwa kulitwaa kombe la Afcon

Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria.

Kocha huyo ni winga wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Barcelona.

Hata hivyo, Amunike amekuwa akilaumiwa na baadhi ya mashabiki kwa namna anavyoteua wachezaji na kupanga kikosi.

Tanzania ilitolewa katika mashindano ya Afcon baada ya kupoteza michezo yote ya makundi.

Soma mengi zaidi

AFCON: Algeria ndio mabingwa wa bara Afrika

Algeria ndio washindi wa kipute cha AFCON mwaka wa 2019 baada ya kuwashinda Senegal 1-0 jijini Cairo.

Senegal ambao hawajawahi kushinda kipute hicho walipewa penalty kunako kipindi cha pili kwa mpira wa mkono lakini ikakataliwa na VAR.

Wachezaji wa Senegal walibubujikwa na machozi baada ya kipenga cha mwisho. Sadio Mane wa Liverpool alionekana mwenye huzuni Algeria walipokua wakisherehekea ushindi wao.

Senegal ambao walikua wakishiriki fainali hio kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2002 walitawala mechi hiyo lakini wakashindwa kufunga.

Kwingineko, meneja wa Inter Milan Antonio Conte anasema Romelu Lukaku ataboresha kikosi chake lakini akakiri kwamba kuna masuala yanayomzuia kumsajiji mshambulizi huyo kutoka Manchester United.

Inter wanamtaka mbelgiji huyo lakini hawajafikia thamani ya United kwa mchezaji huyo, waliyemsajili kwa pauni milioni 75 kutoka Everton miaka miwili iliyopita. Hatachezea United dhidi ya Inter huko Singapore.

Tukisalia Uingereza, kocha wa Arsenal Unai Emery amekiri kwamba mlinzi Laurent Koscielny huenda akaondoka klabuni humo. Raia huyo wa Ufaransa alidinda kujinga na Gunners katika ziara yao ya kabla ya kuanza kwa msimu nchini Marekani na anataka kuruhusiwa kuregea Ufaransa.

Kuondoka kwake kutawacha pengo la uongozi lakini Emery anasema anaona mlinzi Rob Holding kama anaweza kuwa nahodha.

Tukirejea humu nchini, msururu wa raga wa National Sevens unaanza hii leo mjini Kakamega.

Mabingwa Homeboyz watakua wanatafuta kuonyesha ubabe wao watakapofungua kampeni yao dhidi ya wenyeji Western Bulls wakifuatiwa na mechi kati ya Menengai Oilers na Impala. Mwamba wako katika kundi B pamoja  na Nondies, Mean Machine na Kisumu.

Katika kundi C, KCB watachuana na Kisii, Masinde Muliro na Kabra Sugar. Kenya Harlequins wako katika kundi D wakichuana na Nakuru, Strathmore Leos na chuo kikuu cha Egerton.

 

Mastaa watano wakiafrika walioshindwa kulitwaa kombe la Afcon

Dimba la AFCON linafikia kikomo hii leo kule nchini misri huku taifa la Algeria likimenyana na Senegal kwenye mchuano wa Fainali.

Hatahivyo, katika historia ya Afcon, kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.

Wenye mchuano huo macho yote ya mashabiki wa Senegal yataelekezwa kwake Sadio Mane aliyeisaidia Liverpool kutwa kombe la klabu bingwa barani ulaya msimu uliopita.

Riyad Mahrez kwa upande mwingine anatarajiwa kuwaongoza Algeria kutafta taji lake la kwanza kwa taifa lake.

Didier Drogba

htdfs

Barcelona wamewasilisha ofa ya pauni milioni 90 ili kumsajili Neymar

Drogba ameliwakilisha taifa la Ivory Coast kwenye michuano sita ya Afcon.

Kwenye awamu hizo zote alizoiwakilisha Ivory Cokast, Drogba alifika fainali mara mbili huku akipoteza fainali hizo zote kupitia njia ya Penalti. Drogba anakumbukwa sana na mashabiki wa Chelsea kwa goli alilowafunga Bayern Munich mwaka 2012. Katika maisha yake hajawahi shinda taji la Afcon.

George Weah

gfdchx

George Weah ndiye mchezaji bora kuwahi kutokea bara la Afrika. Alikuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka duniani kote ‘Ballon D’ Or’. Weah akiliwakilisha taifa la Liberia hajawahi kulishika taji la Afcon licha ya kukitesa barani ulaya kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Michael Essien

hsdfh

SportPesa yakanusha madai ya kusitisha shughuli zake nchini

Essien alikuwa kiungo mkabaji kutokea taifa la Ghana. Hata hivyo, mkali huyu aliyechezea timu ya Chelsea na Real Madrid alishindwa kuleta taji la AFCON nchini Ghana.

MIchael Essien alikubwa namajeraha ya mara kwa mara jambo lililomkosesha mechi nyingine za AFCON. Atayakumbuka majeraha yake kwa kumkosesha mechi ya robo fainali dhidi ya Uruguay.

Kkatika historia ya Afcon,kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.Kkatika historia ya Afcon,kunao mastaa walliotesa barani ulaya ila wakashindwa kufanyia mataifa yao vivyo hivyo.

Seidou Keita

hgdffs

AFCON: Nigeria wainyuka Tunisia na kumaliza katika nafasi ya tatu

Keita ni mmoja wa viungo bora kuwahi kusakata soka kutoka bara la Africa.

Keita aliwakilisha taifa la Mali kwenye michuano ya Afcon Mara saba huku akishindwa kutwaa taji hilo hata mara moja.

Keita ameshinda taji la klabu bingwa barani ulaya mara mbili na Barcelona ila akirejea nyumbani kwao Mali kitoweo chake kilingia mchanga.

Nwankwo Kanu

th

Licha ya kutwa taji la UEFA pamoja na ligi kuu nchini uingereza, Kanu hakushinda taji la Afcon akiliwakilisha taifa la Nigeria kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2010.

Kanu alistaafu soka la kimataifa baada ya Nigeria kubandul;iwa kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 kule nchini Afrika kusini.

Hata hivyo, Kanu aliliwakilisha taifa la Nigeria kwenye michuano mitatu ya kombe la dunia.

soma mengi hapa

AFCON: Nigeria wainyuka Tunisia na kumaliza katika nafasi ya tatu

Odion Ighalo alifunga bao la pekee Nigeria walipowanyuka Tunisia 1-0 na kumaliza watatu katika kipute cha AFCON mwaka huu.

Ighalo ndiye mfungaji bora wa kipute hicho akiwa na mabao matano. Katika mechi hiyo Tunisia walikaribia kufunga wakati Ferjani Sassi na Ghaylene Chaalali walipopiga mikiki mikubwa.

Misri wajiunga na Nigeria katika 16 bora baada ya kubandua DR Congo

Tunisia walikua mabingwa mwaka wa 2004. Mabingwa mara tatu Nigeria sasa wamemaliza katika nafasi ya tatu mara nane sasa.

Kwingineko, Arsenal wanamsubiri meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane kuidhinisha mkataba wa kiungo wa kati Dani Ceballos. Spurs walikua wanajadiliana na Real kuhusu mchezaji huyo lakini klabu hiyo na mchezaji huyo wanapendelea pendekezo la Gunners la mkopo, huku mkataba ukitarajiwa kuafikiwa kwa baraka zake Zidane.

Real Madrid, ambao pia awali walitaka kumuuza mchezaji huyo, sasa wanataka mkataba wa muda kutokana na mchezaji huyo kuonyesha mchezo mzuri katika michuano ya ubingwa Uropa ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 21.

Nigeria need late Ighalo goal to break down debutants Burundi

Kieran Trippier amejiunga na Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Tottenham. Spurs walipewa fursa ya kumsajili mshambulizi Angel Correa wakati wa majadiliano lakini badala yake wamechagua mkataba wa pesa.

Trippier anaondoka Tottenham baada ya kuwachezea mara 114 katika kipindi cha misimu minne. Mchezaji huyo wa miaka 28 anakua wa nne kusajiliwa na Atletico msimu huu wa joto akijiunga na kina Joao Felix, Marcos Llorente na Felipe ugani Wanda Metropolitano.

Mkataba wake ulikua wa pauni milioni 21.7.

Inter Milan wana shaka kuhusu kitita cha pauni milioni 75 Manchester United inakihitaji kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku.

Inter imetoa ombi la mkopo wa miaka miwili, ambapo wataweza kulipa kwa awamu za Pauni milioni 9, pauni milioni 27 na pauni milioni 27, lakini United wanataka fedha zote kwa mkupuo.

AFCON: Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wabanduliwa

Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano ya AFCON  baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.

Mabao ya Nigeria yalifungwa na Odion Ighalo wa Shanghai Greenland ambaye alicheka na nyavu mara mbili, huku kiungo wa Arsenali, Alex Iwobi akifunga la ushindi.

Misri nao wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.

Kwingineko, Arsenal huenda ikamsaini winga wa Uhispania Lucas Vazquez, 28, kwa mkataba wa pauni milioni 31 kutoka Real Madrid wiki ijayo.

Leicester inaelekea kuvunja rekodi ya uhamisho wa wachezaji kumsajili kiungo wa kati wa Monaco na Ubelgiji Belgium Youri Tielemans,22, ambaye aliyecheza kwa mkopo, uwanja wa King Power karibu nusu ya msimu uliyopita.

 

 

 

Kosa uchekwe! Mechi 5 za AFCON zitakazo kusisimua wikendi hii

Baada ya Kenya kuwa miongoni mwa timu ambazo zilibanduliwa katika kipute cha AFCON wiki hii, raha na vihemko vya mashindano hii zatarajiwa kuongezeka wikendi hii katika mmechi za 16 bora.

Ratba ya mechi za maondoano za AFCON imeshuka na kipute kinaendelea siku ya ijumaa.

Hata hivyo baadhi ya mechi nane ambazo zitapeperushwa kwako kupitia radio jambo, tumekuwekea mechi tano ambazo zitakuwa za kukata na shoka, na ambazi hufai kukosa.

 

Ijumaa, Julai 5

Uganda vs Senegal

Mechi hii ambayo itasakatwa mida ya saa nne, itakuwa ya kukata na shoka kwani majirani hao wetu watakuwa timu ya tatu kutoka Afrika mashariki kupambana na simba wa Teranga.

Inaaminika kuwa kila shabiki kutoka eneo hili la Afrika atakuwa nyuma ya Uganda Cranes.

Mechii hii inawadia pale ambapo wachezaji wa Uganda waliregelea mazoezi yao baada ya kuahidiwa kwamba watalipa dola elfu 6 zaidi kila mmoja, na nchi yao.

Kikosi hicho kiliwasilia uwanjani kuchelewa siku ya jumatano baada ya kuahidiwa pesa hizo.

Wachezaji wa Uganda wamaliza mgomo baada ya kuahidiwa laki sita kila mmoja

Jumamosi, Julai 6

Nigeria vs Cameroon 7PM

Jumamosi pia mashabiki wa soka duniani watakuwa na bahati ya kutazama mechi kali kati ya magwiji wa bara hili, Nigeria ambao ni nambari 3  huku Cameroon ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hili wakiwa nambari 7 katika bara hili.

Jumapili, Julai 7

Madagascar vs DR Congo 7PM

Madagascar ambao wanasakata kipute cha AFCON kwa mara ya kwanza katika historia yao, wamewashangaza wengi kwa mchezo mwema na wa kumezewa mate.

Timu hiyo ambayo inajulikana kama ‘Barea’ ambao ni nambari 108 duniani, waliwanyuka Nigeria katika mechi yao ya mwisho ya kundi B na kufuzu kama viongozi na alama 7.

Watamenyana na DR Congo ambayo ina wachezaji mashuhuri kama Cedric Bakambu, Yannick Bolasie, Chancel Mbemba na Arthur Masuaku Jumapili mida ya saa moja.

Algeria vs Guinea 10PM

Siku hiyo hiyo, Algeria ambao wana mchezaji gwiji Riyad Mahrez wanatarajiwa kucheka na nyavu za Guinea ambao walikuwa miongoni mwa timu nne ambazo zilifuzu kama ‘best losers’ katika kundi B.

Jumatatu, Julai 8

Hata baada ya wikendi kufikia tamati, Jumatatu pia kuna mechi mbili tamu ambazo shabiki sugu wa soka ya Afrika hawezi kosa, kwani hata hautakuwa hoja.

Mali vs Ivory Coast 7pm

Mida ya saa moja, staa wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ambaye anamezewa mate na klabu ya Arsenal atakuwa uwanjani kumenyana na ma staa wa Mali Seydou Keita wa AS Roma na Bakary Sako wa Wolverhampton Wanderers.

Ghana vs Tunisia 10PM

Mechi hii ni moja wapo ya mechi ambazo zinatarajiwa zaidi Afrika na duniani kote, kwani baadhi ya timu hizi mbili kuna mataji 5 ya kombe la bara Afrika.

Je washabikia timu gani?

 

 

Peter Waweru apeperusha bendera ya Kenya katika michuano ya AFCON

 waweru
Sio wengi walipata nafasi ya kusherehekea hadhi hii kwani majirani wetu, Uganda na Tanzania hawakupata nafasi katika orodha hiyo, na kwa hilo tunamsherehekea Peter Waweru.

Harambee Stars yanyukwa na Senegal

Akothee sasa awaomba wachezaji Taifa Stars wampe mimba

Mbwembwe kibao zimetokea baada ya Harambee Stars kuizamisha Taifa Stars ya Tanzania 3-2. Mastaa tofauti katika mitandao ya kijamii wamepata fursa ya kuonyesha mapenzi kwa timu zao. Akothee staa wa kike kutoka nchini hajaachwa nyuma katika mchakato mzima.

Soma hadithi nyingine:

Audio yavuja ! Inasimulia A-Z jinsi mauaji ya William Ruto yatakavyotekelezwa

Staa ya huyu wa kike kupitia mtandao maridhawa wa instagram sasa anadai kuwa anataka ujauzito kutoka kwa vijana hawa wa Tanzania. Akothee sasa ni mama wa watoto 5. Akipata mwingine kwa Taifa Stars sasa atafikisha idadi ya 6.

“I just want to hug all of you when you are back 🤣😂 come here or I come there sweetie 🙏💪💪 mungeshindwa wakenya wangehamia TZ 🤣😂😂😂🤣😂😂😂, Nawafahamu sana watu wangu , hutema watu wao wakishindwa , BRAVOOOOOO BRAVOOOOO , Congratulations TANZANIA ❤ MImi naja huko mnipe ka mimba hapa kenya imekataa .” alisema Akothee.

Tazama hapa:

Akothee sasa anatamba na kibao hatari cha Muje na kinafanya freshi kwenye mtandao wa Youtube na upigwaji mkubwa katika redio na runinga za kitaifa.

Pata hadithi nyingine humu:

Tazama jinsi mastaa na viongozi walivyowapa kongole Harambee Stars

Mastaa kibao hapa nchini na viongozi wametokea pia kuonyesha shavu kubwa kwa timu ya kitaifa akiwemo mheshimiwa Raila Odinga, William Ruto na King Kaka baadhi ya wengineo.

“What a splendid performance #HarambeeStars coupled with great composure coming from behind twice to deservedly win the game. Bravo! Kenyans are firmly rooting for you. All the best as you continue striving to qualify for the #AFCON2019 round of 16. Hongera.” alisema Raila Odinga.

 

Michael ‘Engineer’ Olunga asaidia Kenya kuigaragaza Tanzania

Mabao mawili ya Michael Olunga yaliisaidia Harambee kutoka nyuma na kuwacharaza majirani Tanzania 3-2, katika kipute kinachoendelea cha AFCON nchini Misri, na kusalia kwenye kinyang’anyiro cha 16 bora, kwa mara ya kwanza.

oluu (1)

Wakenya hawapaswi kufikiria Tanzania ni timu ovyo – Ghost Mulee

Tanzania walianza kufunga mabao mawili kupitia kwa Simon Msuva na Mbwana Samatta lakini dakika moja baadae Olunga akasawazisha na kisha kufunga bao la pili kunako dakika ya 80 baada ya Johana Omolo kufunga bao pia, na kuisadia Kenya kupanda hadi katika nafasi ya tatu katika kundi C wakiwa na alama tatu sawia na Senegal.

michael olunga

Awali Algeria walijikatia tikiti ya 16 bora na ushindi wa 1-0 dhidi ya Senegal, kupitia kwa bao la Youcef Belaili.

Tanzania wako chini kwenye orodha hio wakiwa bila ya alama lakini huenda wakafuzu iwapo watawanyuka Senegal katika mechi ya mwisho.

Madagascar nao waliwacharaza Burundi 1-0 na kupanda hadi wa pili katika kundi B wakiwa na alama 4 nyuma ya Nigeria ambao wamefuzu tayari.

Katika msururu wa spoti bara Uropa, Patrick Vieira ni miongoni mwa majina ambayo Newcastle United inatathmini kuchukua nafasi ya Rafael Benitez kama meneja.

Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

Benitez ataondoka St James’ Park baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu ambapo mkataba wake unatamatika tarehe 30 mwezi huu. Mfaransa huyo amemaliza kampeni yake ya kwanza kama meneja wa Nice, na hana haraka ya kuhama lakini atasikiza ofa watakayotoa.

Tukisalia Uingereza, Aaron Wan-Bissaka amemaliza uchunguzi wake wa kimatibabu Manchester United na tangazo maalum kuhusiana na uhamisho wake Old Trafford linatarajiwa kufanya hii leo.

Mlinzi huyo wa miaka 21 alimaliza awamu ya pili ya uchunguzi wake huko Carrington jana kabla ya kuondoka Crystal Palace. Muingereza huyo anakua mchezaji wa pili kusajiliwa na United, baada ya winga wa Wells Daniel James kusajiliwa kutoka Swansea.

AFCON: Mabingwa watetezi Cameroon waanza vyema, Ghana walemewa na Benin

‘Hii ni fainali wasee!’ Mariga ahimiza Harambee Stars kuizaba Tanzania

Siku ya Jumatano, aliyekuwa kiungo wa Harambee Stars, McDonald Mariga alitembelea kikosi cha timu ya taifa mjini Cairo, Misri kabla ya mechi yao dhidi ya Tanzania.

Baada ya Harambee Stars kupoteza mechi yao ya kwanza katika kipute cha kombe la ubingwa bara Afrika dhidi ya Algeria siku ya Jumapili.

Wakenya hawapaswi kufikiria Tanzania ni timu ovyo – Ghost Mulee

Matokeo hayo yaliwacha timu ya taifa ya Kenya katika hali mbaya kwani itabidi wamepata ushindi dhidi ya Tanzania na pia kulazimisha sare dhidi ya Senegal ili kufuzu katika raundi ya 16 bora.

Akijua kibarua ambacho kitawakumba kikosi cha Stars, Mariga alisafiri hadi Misri ili kuwapa motisha kabla ya mechi hiyo ambayo itakuwa kama fainali.

Katika kanda tuliyo iona, Mariga ambaye ni nduguye nahodha Victor Wanyama, aliwahimiza wachezaji hao kusahau matokeo ya mechi iliyopita na kuweka juhudi zote hii leo.

Akizungumza katika lugha ya sheng, Mariga aliwakumbusha kuwa mechi hii ni kama fainali na wanapaswa kuwacha nguvu zote katika uwanja ili kutoka na ushindi.

Ghost Mulee amshauri Victor Wanyama kabla ya kipute cha AFCON

“Hiyo game ya Algeria ishapita watu wasahau. Hii game ya Tanzania tu give hard, hii ni finali wasee, tu deadi kwa uwanjo, kama ni mbaya ni mbaya, hii ni finali. Hakuna kitu ingine.” Alisema Mariga.

Tazama kanda ifuatayo.