Mungu apewe sifa kweli! Kutana na watu maarufu nchini ambao walikuwa ‘Chokoraa’

NA NICKSON TOSI

Watu wengi katika karne ya sasa hutamani sana kuzaliwa katika familia zenye uwezo na wazazi walio na uwezo wa kukithi maslahi yote.

Sio wote ambao ndoto kama hizo hutimia ,kuna wale ambao hupitia katika changamoto na hatimaye kubarikiwa maishani.

Hapa nimekuchorea taswira ya baadhi ya watu ambao walikuwa chokoraa,ama watoto wa kuranda randa mitaani.

Guardian Angel

Ni msanii anayefahamika sana kutokana na nyimbo zake za kuwapa wengi moyo ,na kila mara anapokuwa katika mahojiano na vyomba vya habari mbali mbali ,Guardian hudai kuwa baada ya mamake kufutwa kazi alijikuta katika mitaa ya humu nchini kwani ilimwia vigumu kwa mamake kukimu maslahi yao.

Guardian aidha hutokeza kuwa alitiwa mbaroni na polisi baada ya rais wa tatu wa humu nchini kudai kuwa watoto wote wanaoranda randa mitaani kuondolewa mijini kwani walikuwa wanafanya miji kuonekana michafu.

 

Guardian Angel
Bahati.

Kila mtu natumai kuwa anafahamu historia ya mwanamziki huyo ambaye kwa sasa ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya EMB.

Bahati alijipata katika mitaa ya mabanda ya Mathare baada ya mama mzazi kufariki ,hali iliyomfanya maisha yake kuwa magumu na hata wakati mmoja kujipata katika makao ya kulinda watoto waliofiwa ya ABC Mathare

bahati 2 (1)

Anita Raey.

Mtangazaji huyu wa radio fulani ya humu nchini na mama wa watoto wawili hajawai kosa kusimulia maisha yake yalivyokuwa kabla ya kubarikiwa .

Anita alijipata katika mitaa ya humu nchini kama Chokoraa akiwa na miaka 13  kwa kile alichosema ni kulelewa na mama ambaye alikuwa mkali mithili ya simba na asiyependa kumsikiliza kivyovyote vile.

Kisa ambacho humfanya kutokwa na machozi ni pale alisema kuwa walipokuwa karibu na bustani la Jevanjee wanaume wawili bila ya utu walimnajisi kitu ambacho humfanya kuhuzunika kila mara na hata kuwachukia wanaume maishani.

anita raeyy

Terence Creative aka Kamami.

Terence alizaliwa katika familia ya watoto watatu na yeye alikuwa  kitinda mimba.

Baada ya wazazi wake kufa,Terence akiwa na miaka 9 walilazimika kuishi na Nyanya yao aliyekuwa anaishi katika mitaa ya mabanda ya Mathare.

Kwa wakati mmoja ,alisimulia kuwa alianza kuvuta bangi akiwa na miaka 9 swala lililompelekea kuanza kuwa mwizi na kuanza kuiba vyoo vya magari,pochi za wanawake,na hata kuuza vipuli vya bidhaa zilizozeeka.

Terence.Creative.696x332

Ringtone

Mbali na vituko vyake vya kila mara ambavyo husababisha kwenye mitandao ya kijamii ,Ringtone alikulia pabaya alipokuwa mdogo hali iliyomfanya kuishi katika mitaa ya mabanda  kama chokoraa.

Katika mahojiano na stesheni fulani ,Ringtone alitokeza kuwa mamake alimtupa katika milango ya baa karibu na sanamu ya Tom Mboya ,jiji kuu la Nairobi.

Baada ye Amu wake alimuokota na kumrudisha katika kijiji ambacho mamake alikuwa amezaliwa na kulelewa na Nyanyake.

ringtone

Papa Dennis

Licha ya kwamba ashatangulia mbele ya Mwenye Haki,Papa Dennis atasalia pakubwa katika akili za wengi kutokana na maisha ya utotoni yalivyokuwa.

Papa alilazimika kuacha shule akiwa katika darasa la 8 ,wakiwa wanne bila mtu yeyote wa kuwasetiri maishani walipokuwa wachanga.

Alilazimika kuacha shule na kuingia kwenye mitaa kama chokoraa ili kuwatafutia wadogo wake chakula.

Papa Dennis na kakake Simon
Papa Dennis baada ya kuonyesha talanta ya uimbaji alichukuliwa na mkuu wa shirika la Maliza Umaskini ambaye alimsaidia kwa kurekodi baadhi ya nyimbo zake.

 

PATANISHO: Kama tunarudiana mimi ndio first lady! – Anita

Anita, 26, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na baba mtoto bwana Robert akidai kuwa wawili hao walikosana mwaka wa 2016.

“Alikuwa boy wangu na wakati nilimuambia nina mimba yake ndipo alipoanza kubadilika na kwenda kwake nikapata tayari ana bibi, licha ya kuahidiana kuwa tutaoana.” Alisema Anita.

PATANISHO: Hata alete wanawake kumi I am going nowhere!

Aliongeza,

Imagine Gidi nilimkubali jinsi alivyo hadi nikaharibu kazi yangu kwa kuwa nilikuwa nampenda na akanifanyia hivi. Yule mke wake tulizungumza na nikama alitaka tupigana sasa nikatoka kwa sababu Robert hakuwa.”

Anasema kuwa Roba tangia amkane hajawahi hata mpigia simu kujua jinsi mtoto alivyo. Isitoshe anakiri wazazi wake walimfukuza kwao kwa kupata mimba na yuko tayari kurudiana na Roba hata kama ni kuwa mke wa pili.

Kuna boy tulikuwa tuna push na yeye na akaniambia hawezi oa mtu ana mtoto.

“Wewe si ulianza matusi kuwa mimi ni maskini eti siwezi kusaidia, ulianza hayo matusi hata kabla nioe. Ulimaliza morale kwani ukiniita maskini na kuna mwenye amekubali umaskini wangu nitafanyaje?” Alijitetea Roba.

PATANISHO: Nilioa mwanadada mwenye watoto wawili nikiwa 16

Aliuliza,

Mimi ni hustler, mke wa pili nitatoboa aje?

Robert anasema kuwa atajipanga ajue jinsi atamchukua Anita kama mke wa pili lakini Anita anasema ako tayari kurudiana lakini atatambulika kama mke wa kwanza.

 

Yaani hata Kamami! Tazama picha za mpango wa kando wa Terence Creative

Kupitia mitandao ya kijamii ni wazi kuwa mcheshi Terence Creative ajulikanaye sana kama Kamami ana mpango wa kando na ata amekubali madai ya kuenda nje ya ndoa.

Milly Chebby na mpenzi wake Kamami wamekuwa na misukosuko katika ndoa yao kwa sababu ya kidosho Anita ambaye ndiye mpango wa kando wa bwana Terence.

Baada ya aibu ya Terence kupatikana na mpango wa kando, bwana huyu kupitia mtandao wa kijamii amefungukua wazi na kusema wazi anavyo mpenda mke wake.

Binti ambaye ametia bwana Kamami kwenye aibu chungu nzima ni binti mwenye umri wa miaka 19.

Amini usiamini, mpango wa kando wa bwana Terence ana umri wa miak 19 na wakishirikiana, hawakuwa wanaona kama ni tatizo kwani wahenga walisema, mapenzi ni kipofu!

‘Nilimwagia mpango wa kando wa bwanangu acid,’ Afunguka Mercy

Zaidi ya hayo, hata ikiwa binti huyu amejitia aibu na kumfanya Terence aingie matatani, siwezi kumlaumu bwana Kamami kwani binti huyu Anita ni mrembo sana, yaaani katoto hodari .

Hebu tazama picha

 

Nilimfumania mume wangu na cousin yake kitandani mwetu! – Anita

Wiki hii mtangazaji bi Massawe aliwapa wanawake fursa murwa wafunguke na watoe yaliyo mioyoni mwao kuhus jinsi waume zao waliwacheza kwa kushiriki ngono na jamii zao.
Baadhi ya wengi walijitokeza na kufichua siri ambazo zimefichika miaka na mikaka na hata kama wengi hawakutaka kufichua majina yao, mwanadada mmoja kwa jina Anita hakujali.
Kulingana na Anita kutoka maeneo ya Uthiru, mumewe alimcheza na cousin yake bila aibu!
Akielezea, Anita alisema kuwa siku moja aliporudi nyumbani kutoka kazini, alimfumania mumewe akiwa kitandani na cousin yake. Licha ya kupatikana, mumewe hakujali na Anita alipotaka kujua ni kipi kilikuwa kinaendelea, walizozana na ikageuka kuwa vita.
Hapo ndipo aliamua yameisha na kufunganya virago vyake na kuondoka kwani alijua siku zake kwa ndoa ile zimetamatika.
Aliongeza akisema kuwa aliyekuwa mumewe hujaribu kumpigia simu na kumrai warudiane lakini tendo lile bado humuuma na hakuna jinsi anaweza rudi kwa ile ndoa.
Pata usimulizi wake hapa,

Jinsi ya kuepuka kutongozwa kwenye maeneo ya burudani

Mimi nimewahi pitia hayo mambo! Bwanangu alienda na cousin yake kwani nikienda kazini nilikuwa nawapata wako pamoja.
Siku moja nikawapata kwa bed, kumuuliza ikiwa ni vita so ningefanya nini? Ilibidi niwaondokee.
Hadi wa leo yeye hujaribu kunitafuta lakini hayo machungu bado ninayo.

Kumbe Ni Mrembo Hivi? : Meet Mutula Kilonzo Junior’s Gorgeous Wifey! (PHOTO)

When it comes to his private life, little is known about Makueni County Senator, Mutula Kilonzo Jnr, the son of the late Mutula Kilonzo and brother to lawyer Kethi Kilonzo.

Kilonzo jnr won the senatorial seat after a by election following the demise of his father in 2013. He went on to retain the position in the 2017 general elections.

But what many do not know is that he is a family man. He is married and is a proud father of two kids, a part of his life he has managed to keep under wraps.

However, on Thursday Kenyans got to finally see Mutula’s wife and my! she is gorgeous.

This happened when Mrs. Mutula, who goes by the name Anita Mutula jnr on Twitter, shared a cute selfie photo of her and her hubby in the senate chambers, congratulating her husband during the swearing in of elected members of both houses (Senate and parliament).

My hearty Congratulations on your 2nd swearing in! Proud of you love. May wisdom guide you throughout the term. God bless 🙏

Read Anita’s tweet alongside a photo of the two.

Check out the photo below.

anita.mutula

The post attracted a number of reactions from his followers who like many of us had never seen his wife.

Ralph Ngugi: Senator we can see your stronghold😍😍😍😍

Tona Antonet: Wooow..such a nice couple😘😘Congrats to him Mr senator

Gilbert Kaunda: Heeeee kumbe you’ve a very beautiful wife

Nolle Prose: Am happy for him,he s a mentor n inspire….congrats junior

Jp Owade: A very sober legislator. Keep up the great work sir. Congratulations

John Muia: My Senator!! Apart from politics and your landslide win in Makueni!! Hata wewe umejishindia. “Mundu ekawa undu wikaa!!” Shinda Ushinde.

 

PATANISHO: “Japeth Ni Kama Ana Allergy Ya Wanawake!” – Anita

Hapo jana wanajambo walikuwa mashahidi wa uhondo kamili wakti wa patanisho.

Jamaa kwa jina Japeth aliomba apatanishwe na mkewe Anita ambaye alitoroka nyumbani na mwanao baada ya tabia yake ya kubugia mvinyo kumkasirisha mkewe na kurudi nyumbani baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari

Lakini baada ya mkewe Japeth kupewa nafasi ya kusimulia upande wake , bi Anita aliwashangaza huku akiwachekesha wanajambo baada ya kufichua mengi kumhusu bwanake ambayo hakuwa amesema.

“Ajiheshimu kwanza.” Alifoka Anita.

“Shida sio kulewa kwani nilimpenda vile lakini anapenda wanawake nikama ana allergy ya wanawake. Starehe ndizo anazo chungu nzima ni kama bado hajaamua kufunga ndoa.” Alifichua Anita akisema kuwa mumewe ana tabia mbaya za kuleta wanawake kwake kiholela ili kumuudhi huku akimurai abadilishe mienendo.

“Sijakataa kurudi lakini wacha kwanza nirudi nyumbani nifikirie.” aliongeza anita.

Pata uhondo kamili.